Na. James K.
Mwanamyoto-Geita
Tarehe 17 Desemba, 2021
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema utekelezaji wa miradi ya TASAF unaohimizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan unaendeleza fikra za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere za kuondoa umaskini kwa Watanzania ili waweze kujitegemea.
Akizungumza na walengwa na
wananchi wa Kijiji cha Kanyala mkoani Geita, Mhe. Mchengerwa amesema Mwalimu
Nyerere aliamini taifa haliwezi kujikomboa na kujitawala kwa ufasaha iwapo
kundi kubwa la Watanzania watakuwa tegemezi.
Kutokana na fikra za Baba wa
Taifa, miradi ya TASAF ilibuniwa na Viongozi wa nchi waliotangulia na Mhe. Rais
Samia alipoingia madarakani alitaka kuendeleza fikra hizo ili kuhakikisha kila
Mtanzania anajikomboa kutoka kweye lindi la umaskini.
Mhe. Mchengerwa amesema miradi
ya TASAF tangu ianze, ilitekelezwa kwa asilimia 70 tu ambapo maeneo mengi
yakiwemo ya Mkoa wa Geita hayakuwepo kwenye mpango, lakini Mhe. Rais Samia amedhamiria
kuziingiza kwenye mpango kaya zote zenye sifa zilizobakia ili ziweze kunufaika
na mpango huo na kuhakikisha kila Mtanzania anajitegemea kwa kuinua uchumi wake.
“Hakuna kijiji, kitongoji,
wilaya wala mkoa ambao hautaguswa na fedha ambazo Mhe. Rais anazitoa ili
kuhakikisha kila Mtanzania anajitegemea, hivyo tutuwajengee uwezo, tuwakomboe
katika uchumi wa mtu mmoja mmoja ili kuondoa umaskini,” Mhe. Mchengerwa
amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa yuko mkoani
Geita kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji
kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha
Kanyala wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya
TASAF mkoani Geita.
Umati wa walengwa wa TASAF na wananchi wa
Kijiji cha Kanyala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa akizungumza
nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
mkoani Geita.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Emmanuel Macha akizungumza na walengwa wa
TASAF na wananchi wa Kijiji cha Kanyala kwenye ziara ya kikazi ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kanyala wanaodai
kutoingizwa kwenye Mpango wa TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.
Mratibu
wa TASAF wa Halmashauri ya Mji-Geita, Bi. Upendo Kilonge akitekeleza maelekezo
ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ya kuandika majina ya wananchi wa Kijiji cha
Kanyala wanaodai kutoingizwa kwenye Mpango wa TASAF wakati wa ziara ya kikazi
ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akimpongeza mlengwa wa TASAF wa Kijiji cha Kanyala
aliyetumia vizuri ruzuku yake kwa kufungua duka ili kumudu kuendesha maisha
yake wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
mkoani Geita.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akimsikiliza mlengwa wa TASAF wa Kijiji cha Kanyala
aliyetumia vizuri ruzuku yake kujenga nyumba, choo bora na kuchimba kisima wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.
No comments:
Post a Comment