Na. James K.
Mwanamyoto-Kagera
Tarehe 18 Desemba, 2021
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amemuelekeza
Katibu Mkuu-UTUMISHI, kumuondoa kwenye nafasi yake Afisa Manunuzi Mkuu wa
TARURA ili kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha za miradi.
Waziri Mchengerwa ametoa
maelekezo hayo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani
humo.
Mhe. Mchengerwa amesema,
uamuzi wa kumuondoa mtumishi huyo, unatokana na taarifa za uwepo wa mikataba
mingi iliyosainiwa na baada ya muda ikafanyiwa mapitio na kuongezwa fedha jambo
ambalo ni kinyume na utaratibu.
“Wakati uchunguzi unaendelea,
Afisa Manunuzi Mkuu huyo aripoti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora siku ya Jumatatu tarehe 20 Desemba, 2021 na apelekwe Afisa
mwingine atakayetekeleza majukumu yake,” Mhe. Mchengerwa ameongeza.
Aidha, amemuelekeza Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU kupitia mikataba yote ya TARURA na kuchukua hatua stahiki pale
itakapothibitika kuna ubadhirifu wa fedha.
“Namuelekeza Mkurugenzi Mkuu
wa TAKUKURU kwenda TARURA kupitia mikataba yote kwa makini ili achukue hatua
stahiki kwa watendaji ambao wanashiriki vitendo vya ubadhirifu vinavyokwamisha
taifa kusonga mbele,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa amesema kama
taifa, ni lazima kufanya maamuzi magumu pale inapobidi ili nchi iweze kupiga
hatua katika maendeleo na wananchi wanufaike.
Amesema, Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan alipofungua fursa za kiuchumi katika utekelezaji wa miradi ya
serikali, alitaka taifa lipige hatua katika maendeleo na sio watu wafanye
ubadhirifu wa fedha za umma, hivyo tumuunge mkono kwa kupinga vitendo
vinavyorudisha nyuma maendeleo.
Mhe. Mchengerwa amesisitiza
kuwa, Watumishi wa Umma hawana sababu ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa
na ubadhirifu kwasababu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anajali maslahi yao na yeye
ni msikivu kwa watumishi.
Mhe. Mchengerwa amefanya ziara
ya kikazi ya siku moja mkoani Kagera ambapo amezungumzat na watumishi, walengwa
wa TASAF na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Umma wa Mkoa wa
Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa
Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Kagera.
Sehemu
ya Viongozi na Watumishi wa Umma wa Umma wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Kagera.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akijadiliana jambo na
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ACP
Ibrahim Mahumi wakati wa kikao kazi cha Mhe. Mchengerwa na Viongozi na
Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kagera.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akifafanua hoja zilizowasilishwa na Watumishi wa Mkoa wa Kagera
wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa mkoa huo kilicholenga kuhimiza
uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
mkoani humo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, ACP Ibrahim Mahumi akitoa
ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed
Mchengerwa na watumishi wa Mkoa wa Kagera kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa
Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akitunuku cheti cha utambuzi wa utendaji kazi mzuri kwa
mtumishi wa Mkoa wa Kagera, Bi. Maria Valentine-Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja
la II, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa
Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment