Na. Veronica Mwafisi-Mkuranga
Tarehe 28 Disemba, 2021
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi ameonya vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watumishi
wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza
na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga katika kikao kazi chake na
watumishi hao, Mhe. Ndejembi amewataka kujirekebisha na kufanya kazi kwa
uadilifu na weledi ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima inayosababishwa na
utendaji kazi wao usioridhisha.
Ameongeza
kuwa, watumishi wa Idara hiyo ya ardhi wakiendelea na utamaduni wa kufanya kazi
kwa kuweka maslahi binafsi mbele wataipotezea Serikali mapato na kuwanyima haki
wananchi wa Mkuranga kupata maendeleo yanayotokana na kodi itayokusanywa na
Serikali katika Halmashauri hiyo.
Akisisitiza
uadilifu kwa watumishi hao, Mhe.Ndejembi amewataka wabadilike kwa sababu
wamekuwa wakilalamikiwa kuwaonea wananchi kwa kuwaomba rushwa na kutowashauri
vizuri kwenye masuala yanayohusu umiliki wa ardhi.
“Nimeambiwa
hapa Mkuranga hata mimi nikihitaji shamba natakiwa kuwa na kitu kidogo cha
kuwapatia watumishi wa Idara ya ardhi ambao wameweka maslahi yao binafsi mbele,
na wala sitaki kumtaja mtu mmoja mmoja hapa zaidi ya kuwasisitiza mbadilike”,
Mhe. Ndejembi amefafanua.
Kuhusiana
na migogoro inayoibuka, Mhe. Ndejembi amewataka Watumishi wa Idara hiyo kuwa
watatuzi wa migogoro badala ya kuwa chanzo cha migogoro.
Mhe.
Mhe. Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya
Wilaya ya Mkuranga yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma wa
Halmashauri hiyo, ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa
Kuzinusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF).
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji.
Baadhi
ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakimsikiliza Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao wilayani
Mkuranga chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Ali akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na watumishi wa umma wa
Halmashauri hiyo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la
kuhimiza uwajibikaji.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akisikiliza hoja ya mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mkuranga (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa
Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mtumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi. Jessy Mpangala akiwasilisha changamoto
ya kiutumishi inayomkabili kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akiwahimiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga
kutumia mfumo wa SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI kwa kuwasikilizisha makala fupi ya
picha za mwendo (video clip) inayotoa muongozo wa namna ya kutumia mfumo huo,
wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi. Mwantum Mgonja akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji ya halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Watumishi wa Halmashauri hiyo
chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment