Na.
James K. Mwanamyoto-Dodoma
Tarehe
06 Mei, 2021
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael amesema,
Serikali kupitia Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu imeandaa rasimu ya
Mwongozo wa Kitaifa wa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma
utakaowezesha kuainisha mahitaji sahihi ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kuwezesha
usimamizi na matumizi mazuri ya rasilimaliwatu.
Dkt.
Michael amesema hayo leo jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI wakati
akifungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma.
Dkt.
Michael amesema, bila kuwa na mpango wa rasilimaliwatu, Serikali inaweza kupata changamoto ya
upungufu wa watumishi au kuwa na watumishi wengi wanaotosheleza kwa idadi
lakini hawana ujuzi wa kutekeleza majukumu yao kikamilifu, hivyo ndio maana
Serikali imeona umuhimu wa kuhuisha Mpango wa Rasilimaliwatu wa Kitaifa.
Amefafanua
kuwa, ili kufikia uchumi wa kati wa juu kupitia Sera ya Maendeleo ya Viwanda ni
dhahiri kuwa Utumishi wa Umma unapaswa kuwa na watumishi wa kutosha na wenye
sifa stahiki hivyo amewataka washiriki kutumia uzoefu wao kujadili kwa kina rasimu
ya mpango huo kwa lengo la kuiwezesha Serikali kupata mwongozo mzuri wa kuandaa
Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu utakaokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa.
Tumieni
uzoefu wenu na elimu mliyonayo pamoja na ubunifu ili kuiwezesha Serikali kupata
Mpango Mzuri wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu. Dkt. Michael amesisitiza.
Kwa
upande wa washiriki, Mkurugenzi Msaidizi Utawala wa Wizara ya Maji Bi. Wanyenda
Kuta amesema, Mpango huo wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu utawezesha Utumishi wa
Umma nchini kuwa na rasilimaliwatu yenye sifa na kukidhi utoaji wa huduma bora
kwa wananchi.
Naye,
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimaliwatu TAMISEMI, Bw. Marko Masaya amesema kuwa,
Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu utaziwezesha Taasisi za Umma kuandaa
mipango ya kati, muda mfupi na mrefu
itakayosaidia kuwa na watumishi wenye sifa stahiki na malengo
yanayopimika na kuongeza kuwa utawezesha kujua aina ya watumishi wanaohitajika
na sehemu watakayopatikana aidha ndani au nje ya Utumishi wa Umma.
Sanjali
na hilo, Bw. Masaya ameongeza kuwa, mpango huo utaiwezesha Serikali kujua
katika kipindi cha miaka miwili au mitatu ijayo itahitaji kuwa na watumishi wa
aina gani, wenye weledi upi na kiwango kipi cha elimu.
Kikao
cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa
Umma kimejumuisha wasimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka katika Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa
na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Naibu Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael akifungua
kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Washiriki
wa kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) wakati akifungua kikao
hicho kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Bw. Elisante Mbwilo
akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, Dkt. Francis Michael kufungua kikao cha kujadili rasimu ya Mpango wa
Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika leo jijini
Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Dkt. Edith Rwiza akiwasilisha mada
kuhusu Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu kwa Washiriki wa kikao cha kujadili
rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Francis
Michael akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kujadili rasimu
ya Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma baada ya
kufungua kikao hicho kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Msaidizi Utawala wa Wizara ya Maji Bi. Wanyenda Kuta akizungumzia matarajio
yake kuhusu Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu unaojadiliwa jijini Dodoma na
wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma.
Mkurugenzi
Msaidizi Rasilimaliwatu TAMISEMI Bw. Marko Masaya akizungumzia umuhimu wa
Mpango wa Kitaifa wa Rasilimaliwatu unaojadiliwa na unaojadiliwa jijini Dodoma
na wadau kutoka katika Taasisi mbalimbali za Umma.
No comments:
Post a Comment