Na. James K. Mwanamyoto-Mpanda na Tanganyika
Tarehe 29 Mei, 2021
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean
Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma waliopewa dhamana ya kuwasimamia na
kuwaongoza watumishi walio chini yao kutambua kwamba, cheo ni dhamana, hivyo wanapaswa
kutumia vyeo vyao vizuri kuwahudumia wananchi na wanaowasimamia badala ya
kujikweza.
Dkt. Ndumbaro ametoa wito huo kwa Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi, Manispaa ya Mpanda na Halmashauri za Wilaya ya Nsimbo na Tanganyika wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Katavi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi walio katika maeneo ya pembezoni mwa nchi.
Amesema hakuna haja ya wenye madaraka katika Utumishi wa Umma kuwakandamiza waliochini yao, bali wanapaswa kutengeneza mazingira ya amani mahala pa kazi ili wao na wanaowasimamia washiriki kuujenga utumishi wa umma wenye msingi imara wa maadili na unaozingatia Kanuni, Sheria, Taratibu na Miongozo iliyopo.
“Mamlaka uliyonayo katika utumishi wa umma si lazima uyaonyeshe kwa mabavu na kujikweza kwani jamii inatambua na kukuheshimu kwa cheo au nafasi uliyonayo”, Dkt. Ndumbaro amesisitiza.
Ameongeza kuwa, cheo ni kama koti tu kwani ipo siku utalivua na litavaliwa na mwingine aidha kwa kustaafu au Serikali kumpatia mwingine cheo hicho, hivyo amewataka watumishi waliopo mkoani au makao makuu ya taasisi yoyote ile kutojiona kuwa ni bora kuliko wengine.
Amewakumbusha viongozi waliopo katika utumishi wa umma kuwahudumia wengine vizuri ili pindi watakapostaafu na kurejea kupata huduma katika ofisi walizokuwa wakiziongoza wapokelewe kwa heshima na kuhudumiwa vizuri.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Abdallah Malela amesisitiza utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Dkt. Ndumbaro kwa kuwataka Watumishi wa Umma mkoani Katavi kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo mkubwa na kuongeza kuwa, huo ndio utamaduni unaopaswa kuzingatiwa na mtumishi yeyote wa umma.
Dkt. Ndumbaro amehitimisha ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi kwenye halmashauri zilizopo pembezoni, ziara ambayo ililenga kuhimiza utendaji kazi wenye matokeo ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anautaka katika utawala wake, Sanjali na hilo Dkt. Ndumbaro ametumia ziara hiyo kutatua changamoto na kero zinazowakabili Watumishi wa Umma waliopo maeneo ya pembezoni katika mikoa hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean
Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Tanganyika wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Katavi yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi
walio katika maeneo ya pembezoni.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tanganyika wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati wa ziara yake ya kikazi yenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji pamoja na kusikiliza na kutatua kero na
changamoto zinazowakabili watumishi walio katika wilaya hiyo.
Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Tanganyika Bw. Omari Himidi akiwasilisha changamoto yake ya kiutumishi kwa Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro
wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili
watumishi walio katika wilaya hiyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Katavi, Manispaa ya Mpanda na Halmashauri za Wilaya ya Nsimbo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Katavi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji pamoja na kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi walio katika maeneo ya pembezoni mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Bw. Abdallah
Mohamed Malela akimshukuru Dkt. Laurean Ndumbaro kwa kufanya ziara ya kikazi
mkoani Katavi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji pamoja na kusikiliza na
kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi walio katika maeneo ya
pembezoni mkoani humo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa
Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akitoa
huduma kwa mtumishi aliyewasilisha changamoto ya kiutumishi mkoani Katavi
wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Laurean Ndumbaro yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi walio katika
maeneo ya pembezoni mkoani humo.
Katibu wa Afya Mkoa wa Katavi Bw. Apolinari
Mushi akiwasilisha changamoto za kiutumishi kwa Katibu Mkuu Utumishi, Dkt.
Laurean Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Katavi
yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji pamoja na kusikiliza na kutatua kero na
changamoto zinazowakabili watumishi walio katika maeneo ya pembezoni mkoani
humo.
No comments:
Post a Comment