Na. James K.
Mwanamyoto-Zanzibar
Tarehe 12 Mei, 2021
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amezitaka taasisi za kifedha nchini kutoa mikopo kwa wananchi wenye hatimiliki za kimila zinazotolewa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) ili kuwawezesha wananchi hao kuendesha shughuli zao na kuinua kipato.
Akikabidhi
hatimiliki hizo kwa baadhi ya wananchi wa Shehia ya Welezo, Zanzibar, Mhe.
Mchengerwa amesema, hatimiliki hizo zinalenga kutoa fursa kwa wananchi kupata
mikopo itayowawezesha kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na biashara
ili kuboresha maisha yao.
“Taasisi
za kifedha zitambue hatimiliki hizi na kupunguza masharti ili kuwawezesha wafanyabiashara
wadogo kukopa na kuongeza mtaji.” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Akiwa katika kituo Jumuishi
cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kilichoko katika Baraza la Biashara,
eneo la Darajani Wilaya ya Mjini, Mhe. Mchengerwa amezitaka pia taasisi za
kifedha kutoa mikopo kwa wajasiriamali waliorasimisha biashara zao na kuongeza
kuwa, mikopo hiyo itawaongezea mitaji ya kuendesha shughuli zao za ujasiriamali.
Kutokana na uwepo wa kituo
hicho, Mhe. Mchengerwa amehimiza zoezi la urasimishaji biashara lisichukue muda
mrefu ili kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kurasimisha biashara
zao.
Akieleza mchango wa ofisi yake
katika zoezi la urasimishaji biashara, Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na
Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Dkt. Islam Seif Salum amesema kituo hicho
kimejengwa ili kuondoa changamoto za urasimishaji walizokuwa wakikutana nazo wafanyabiashara
wadogo.
Dkt. Salum ameongeza kuwa
kutokana na faida za uwepo wa kituo hiki, Serikali imedhamiria kujenga kituo
kama hiki Pemba ili wananchi wa eneo hilo nao waweze kunufaika.
Naye Mratibu wa Mkurabita,
Dkt. Seraphia Mgembe amesema utekelezaji wa MKURABITA Zanzibar umewanufaisha
wananchi wa Zanzibar kwa kuwapatia mafunzo ya utunzaji wa kumbukumbu za
biashara ambapo hivi sasa wanazo takwimu sahihi za maendeleo ya biashara zao.
Mhe. Mchengerwa amehitimisha
ziara yake ya kikazi Zanzibar ya kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi
zilizo chini ya ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa Sekretarieti ya Ajira ofisi ya Zanzibar.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa Shehia ya Welezo wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya MKURABITA, Zanzibar.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akitoa hatimiliki kwa mmoja wa wananchi wa Shehia ya Welezo
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya MKURABITA,
Zanzibar.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na wajasiriamali (hawapo pichani) wanaopata
huduma katika kituo Jumuishi cha
Urasimishaji na Uendelezaji Biashara kilichoko katika Baraza la Biashara, eneo
la Darajani Wilaya ya Mjini wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya MKURABITA, Zanzibar. Kulia kwake ni Katibu
Mkuu, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Dkt. Islam Seif
Salum.
Baadhi
ya Wajasiriamali wa Zanzibar waliorasimisha biashara zao kupitia kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara
kilichoko katika Baraza la Biashara, eneo la Darajani Wilaya ya Mjini
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
ya kikazi ya Waziri huyo Zanzibar.
Mratibu
wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania
(MKURABITA), Dkt. Seraphia Mgembe akitoa taarifa ya utekelezaji ya kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara
kilichoko katika Baraza la Biashara eneo la Darajani Wilaya ya Mjini, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya MKURABITA, Zanzibar.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akihimiza zoezi la urasimishaji wa biashara kufanyika kwa
wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi katika kituo Jumuishi cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara
kilichoko katika Baraza la Biashara, eneo la Darajani Wilaya ya Mjini.
Wanaomsikiliza ni Watendaji wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda
Zanzibar na Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe.
No comments:
Post a Comment