Na. James K.
Mwanamyoto-Dar es Salaam
Tarehe 19 Mei, 2021
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) kutotoa siri za wananchi wanaowasilisha taarifa za uwepo wa vitendo vya rushwa kwenye taasisi hiyo ili ziweze kufanyiwa kazi.
Akizungumza wakati wa kikao
kazi chake na Viongozi wa TAKUKURU leo jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa
amemuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni
kuhakikisha vyanzo vya taarifa za rushwa vinalindwa ili kuhamashisha wananchi
kuendelea kutoa taarifa zitakazoiwezesha Serikali kulinda rasilimali za taifa.
Mhe. Mchengerwa amehimiza
uadilifu kwa Watumishi wa TAKUKURU hususan kwenye eneo la utunzaji siri za
watoa taarifa ili kuwajengea wananchi imani ya kuendelea kushirikiana na
TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa.
“Utoaji wa siri za
wanaowasilisha taarifa za vitendo vya rushwa, unahatarisha usalama wao, hivyo
Mkurugenzi Mkuu uanze na suala hili ili tubaini watumishi wote wanaotoa siri za
watoa taarifa na kuwachukulia hatua za kinidhamu.” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe. Mchengerwa amewaasa
watumishi hao kutenda haki wanaposhughulikia vitendo vya rushwa ili kutoitia
dosari Ofisi hiyo inayoaminiwa na wananchi.
Kuhusu utekelezaji wa
maelekezo ya Mhe. Rais juu ya taasisi hiyo kujikita moja kwa moja katika
majukumu yake, Mhe. Mchengerwa amewakumbusha Viongozi hao kutekeleza maelekezo hayo
ipasavyo kwa kushughulikia masuala yanayohusiana na rushwa, ubadhirifu wa mali
za umma na uhujumu uchumi na si vinginevyo.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema,
Serikali ina imani na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Hamduni na Naibu
wake Bi. Neema Mwakalyelye walioapishwa leo na Mhe. Rais, na ndio maana
wamepewa dhamana ya kuiongoza taasisi hiyo nyeti.
Akizungumza na viongozi wa TAKUKURU kabla ya kumkaribisha Mhe. Mchengerwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewahimiza watendaji wa TAKUKURU kutofanya kazi zisizoihusu TAKUKURU kama ambavyo Mhe. Rais na Waziri Mchengerwa wamekuwa wasisitiza.
Mhe. Ndejembi ameitaka
TAKUKURU kuhakikisha inayakamilisha kwa wakati mashauri ya msingi yanayoihusu taasisi
hiyo na kwa yale yasiyokuwa na msingi yafutwe ili kutoa fursa kwa taasisi hiyo kuendelea
kutekeleza majukumu yenye tija kwa taifa.
Kwa upande wake. Mkurugenzi wa
TAKUKURU, CP Salum Hamduni amekiri kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri na kuahidi
kuyafanyia kazi ndani ya muda aliolekeza.
Ili kutekeleza maelekezo ya
Mhe. Mchengerwa kwa wakati, CP Hamduni amewataka watumishi wake kujitoa
kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu ya TAKUKURU ili kufikia malengo ya
taasisi hiyo.
Mhe. Mchengerwa amefanya kikao
kazi na Viongozi wa TAKUKURU mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo na
Naibu wake kuapishwa na Mhe. Rais-Ikulu Jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kuhimiza
uwajibikaji na utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais aliyedhamiria taasisi hiyo
kutekeleza majukumu yake kwa weledi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akikaribishwa na
Watumishi wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam alipowasili kwa ajili ya kikao
kazi chake na Viongozi wa TAKUKURU kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisalimiana na
Watumishi wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam alipowasili kwa ajili ya kikao
kazi chake na Viongozi wa TAKUKURU kilicholenga kuhimiza uwajibikaji. Kulia
kwake Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi na Viongozi Wakuu wa TAKUKURU
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Mohamed Mchengerwa akizungumza na Viongozi wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam
wakati wa kikao kazi chake na Viongozi hao chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji. Kulia kwake ni Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi na
kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika kikao
kazi na Viongozi wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza kabla
ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzungumza na Viongozi wa TAKUKURU leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum
Hamduni akiahidi kutekeleza maelekezo aliyopewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa
wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Viongozi wa TAKUKURU leo Jijini Dar es
Salaam chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akionyesha nembo
ya TAKUKURU aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni baada
ya kikao kazi cha Waziri huyo na Viongozi wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam
chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi wa TAKUKURU mara baada ya kikao kazi cha Waziri huyo na
Viongozi hao wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji. Kulia kwake ni Naibu Waziri wake, Mhe. Deogratius Ndejembi na
kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiagana na
Viongozi Wakuu wa TAKUKURU mara baada ya kikao kazi cha Waziri huyo na Viongozi
hao wa TAKUKURU leo Jijini Dar es Salaam chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment