Friday, October 4, 2019

WATUMISHI WA UMMA NCHINI WATAKIWA KUTUMIA VIZURI RASILIMALI KATIKA UTENDAJI KAZI WAO


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu Mkoani  Mwanza. Kulia ni Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Balozi Mstaafu Mhe. John Haule, Mhe. Khadija Mbarak na Mhe. Alhaj Yahya Mbila.

Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu Mkoani  Mwanza.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu kabla ya kikao kazi kati yake na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Dkt. Philemon Sengati wakati wa kikao kazi kati yake na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu.

Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Balozi Mstaafu Mhe.John Haule, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma, wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza  kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu.

No comments:

Post a Comment