Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na baadhi ya Watendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Momba na Tunduma mkoani Songwe jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kukagua
utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara
za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na kuzungumza na watumishi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Ardhi, Bw. Kelvin
Joseph alipokuwa akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi wa urasimishaji
mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa
Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA). Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Momba, Mhe. Juma Irando.
|
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maelekezo ya namna ya kuwaunganisha
wanufaika wa MKURABITA na taasisi za fedha ili waweze kupata mikopo na kujiinua
kiuchumi wakati Naibu Waziri huyo aliposimama kukagua utekelezaji wa Mradi wa
urasimishaji mashamba ya wakulima katika Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba
Mkoa wa Songwe katika ziara yake ya kikazi mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara
za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
|
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara
za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) wa Kijiji cha Naming’ongo wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake ya kikazi
mkoani humo jana ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Mpango huo.
|
No comments:
Post a Comment