Tuesday, October 8, 2019

RUZUKU YA TASAF YABORESHA MAISHA YA WANAKIJIJI WA MKWANDA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bw. Adam S. Mboka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.

Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bi. Aisha Jongo akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyoyapata kupitia TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo wilayani humo yenye lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.

Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bw. Issa Shaban Mfaume akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyoyapata kupitia TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo wilayani humo yenye lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisoma bango linaloutambulisha Mradi wa Bwawa la Samaki unaotekelezwa na wanufaika 82 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru alipoutembelea mradi huo kwa lengo la kujionea shughuli zinatofanywa na wanufaika hao.

Mradi wa Bwawa la Samaki unaotekelezwa na wanufaika 82 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametembelea mradi huo.

No comments:

Post a Comment