Saturday, October 5, 2019

WANANCHI WA VIJIJI VYA TUPENDANE, MTANGALANGA NA KITONGOJI CHA AMKENI KATIKA HALMASHAURI YA MJI NEWALA KUNUFAIKA NA ZAHANATI ILIYOJENGWA NA TASAF

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Kulia) akishuhudia jiwe la msingi la Zahanati ya Tupendane iliyojengwa na TASAF, mara baada ya Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2019, Ndugu Mzee Mkongea Ali (kushoto) kuweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo. Mwenge wa Uhuru uliwasili juzi katika Halmashauri hiyo ya Mji Newala.

Mwenge wa Uhuru ukiwa mbele ya Zahanati ya Tupendane iliyojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mara baada ya ujumbe wa Mwenge huo kuitembelea Halmashauri ya Mji Newala ili  kukagua na kujiridhisha na ujenzi wa zahanati hiyo. Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2019, Ndugu Mzee Mkongea Ali ameweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo.

Sehemu ya viongozi na wananchi wa kijiji cha Tupendane katika Halmashauri ya Mji Newala waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya  ujumbe wa Mwenge huo kuwasili kwa ajili ya  ukaguzi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho. 



No comments:

Post a Comment