Tuesday, October 8, 2019

DKT. MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA KUTOOMBA UHAMISHO BILA KUWA NA SABABU ZA MSINGI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu  (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Balozi Mstaafu John Haule.

Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo.

Muuguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Dalahile Malele akiwasilisha malalamiko yake kuhusu kutojibiwa kwa maombi yake ya uhamisho wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni kabla ya kikao chake na watumishi wa Halmashari ya Wilaya ya Itilima kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.


No comments:

Post a Comment