Na
Happiness Shayo- MEATU
Serikali
imewataka waajiri nchini kuweka kipaumbele katika programu za mafunzo kwa Watumishi wa Umma ili
kuwajengea uwezo kiutendaji kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya kiutendaji.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi chake na
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu
kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.
“Waajiri
hakikisheni mnatoa mafunzo kwa watumishi wenu ili kuendana na kasi ya Sayansi
na Teknolojia ikiwa ni pamoja na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Dkt.
Mwanjelwa ametoa wito huo baada ya kubaini kuwepo kwa uelewa mdogo wa masuala
ya kiutumishi kwa baadhi ya watumishi wa umma wilayani humo.
“Nimegundua
bado kuna ombwe la uelewa mdogo wa miiko ya kazi miongoni mwa watumishi wa umma
unaosababisha kufanya kazi kwa mazoea, hivyo mafunzo yatawasaidia kuboresha
utendaji kazi wao.” Dkt. Mwanjelwa ameongeza.
Aidha,
Dkt. Mwanjelwa ameitaka Tume ya
Utumishi wa Umma kuwa na utaratibu wa kujiridhisha kama Waajiri wanawapeleka
watumishi kupata mafunzo katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ili wawe na
ufanisi kiutendaji.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa
kufanya ziara wilayani hapo na kuahidi kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa.
Dkt.
Mwanjelwa amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji na
watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za watumishi hao na
kuzitatua.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa
(Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani
Simiyu (hawapo pichani) wakati wa
kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa
Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Umma
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
Mkoani Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo.
Afisa Utumishi Mwandamizi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Elisha Msengi akijibu hoja wakati wa kikao kazi kati ya Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Meatu kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.
No comments:
Post a Comment