Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 27 Februari, 2025
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha
Mshahara kuwasilisha mapendekezo ya Kima cha chini cha mshahara yanayochozingatia
hali halisi ya maisha na maslahi ya wafanyakazi ili kuepuka migogoro na kushuka
kwa morali ya wafanyakazi, tija na uzalishaji.
Mhe.
Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa
Umma.
Mhe. Simbachawene amesema Kima cha Chini cha Mshahara
ni suala muhimu sana na lisiposhughulikiwa vizuri linaweza kusababisha migogoro
isiyo ya lazima na hivyo kuzorotesha uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Ameongeza kuwa, Kima cha chini cha mshahara
kisichozingatia hali halisi ya uchumi ni hatari katika maendeleo ya nchi hasa
kutokana na ukweli kwamba kunaweza kusababisha kutokea kwa mfumuko wa bei, na
kuongeza gharama za uendeshaji.
Waziri Simbachawene amesema Bodi ya Mshahara katika
Sekta ya Umma ina jukumu la kufanya uchunguzi na kupendekeza kwa Waziri mwenye
dhamana na masuala ya Utumishi wa Umma kuhusu Kima cha Chini cha Mshahara
katika Sekta ya Umma, hivyo katika kutekeleza majukumu haya, Bodi ina wajibu wa
kuzingatia maslahi ya nchi na mustakabali wa uchumi wa nchi wakati wa kutoa
mapendekezo stahiki.
Kwa
Upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi
wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda amesema
pamoja na uzinduzi wa bodi hiyo, Wajumbe watapatiwa mafunzo kwa ajili ya kujengewa
uwezo zaidi na kupata uelewa kuhusu majukumu ya upangaji wa kima cha chini cha
mshahara katika Utumishi wa Umma.
Naye Mwenyekiti
wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma, Bw. Mathias
Kabunduguru amemuahidi Waziri Simbachawene kuwa watatekeleza majukumu yao kwa
ufanisi na malengo yaliyokusudiwa katika kupendekeza na kutoa ushauri kwa
ustawi wa nchi.
Uteuzi wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara umefanywa
kwa mujibu wa Kifungu cha 35(1) cha Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka
2004 na kufanyiwa marekebisho kupitia kifungu cha 14(b) cha Sheria ya Marekebisho
ya Sheria ya Ajira na Kazi (The Employment and Labor Laws (Miscellaneous
Amendment Act) Na. 24 ya mwaka 2015.
Kupitia
Marekebisho hayo yaliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tarehe 08/07/2015, Serikali ilianzisha Bodi mbili, moja kwa ajili ya Sekta
binafsi na nyingine kwa ajili ya Sekta ya Umma. Marekebisho hayo yalilenga
kuboresha ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha uzinduzi wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa
Umma kilichofanyika jijini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi
wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene
wakati akizindua bodi hiyo kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Taasisi, Bw. Nolasco Kipanda akitoa
maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzindua
Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma kwenye kikao
kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi
ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma wakiwa kwenye kikao cha
uzinduzi wa bodi hiyo uliozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma, Bw. Mathias Kabunduguru akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya Waziri huyo kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Bodi
ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizindua bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikabidhi vitendea kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma Bw. Mathias Kabunduguru mara baada ya kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha
na Marupurupu, Bi. Mariam Mwanilwa mara baada ya Waziri huyo kuwasili kwa lengo
la kuzindua Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara katika
Utumishi wa Umma jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati mstari wa mbele) akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya
Kima cha Chini cha Mshahara katika Utumishi wa Umma baada ya kuzindua bodi hiyo jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment