Na Mwandishi Wetu-Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametoa maelekezo tisa kwa
lengo la kuboresha Utumishi wa Umma ikiwamo kuwataka Wakuu wa Taasisi za Umma
kuchukua hatua stahiki pale maadili yanapothibitika kuwa yamekiukwa na
watumishi.
Mhe. Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu Machi 3, 2025 jijini Dodoma wakati akifungua
Kikao Kazi kati yake na Wakuu wa Taasisi za Umma.
Amesema ni vyema Wakuu wa Taasisi za Umma kuendelea
kusimamia utawala na rasilimaliwatu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika Utumishi wa Umma.
Pia, Mhe. Simbachawene amewataka Wakuu hao wa Taasisi kuhakikisha Ofisi zao zinajiunga na kutumia
kikamilifu mifumo ya kidijiti ya kiutumishi iliyosanifiwa
na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Amesema taarifa za Watumishi zilizopo katika Mfumo
Jumuishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (e-Watumishi) zisafishwe kwa
ajili ya kuwezesha kufanyika kwa maamuzi sahihi ya masuala mbalimbali ya
kiutumishi.
Mhe. Simbachawerne amewasisitiza Wakuu hao wa Taasisi kuacha kuwasilisha au kupitisha
nakala ngumu za barua za maombi ya masuala ya kiutumishi ambayo kwa sasa
yanashughulikiwa kupitia mifumo ya kidijiti.
Aidha, amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za
Mitaa kutenga nafasi za ajira mpya kwa kuzingatia maelekezo ya mwongozo wa
maandalizi ya ikama na bajeti hususan kwenye maeneo ya rasilimaliwatu yenye
upungufu mkubwa na ambayo ni kipaumbele cha Serikali katika kutoa huduma bora
kwa wananchi.
‘’Watumishi wanaopangiwa katika vituo vyenu vya kazi
au waliohamishiwa katika taasisi zenu muwapokee kwa mujibu wa maelekezo pamoja
na kuwachukulia hatua stahiki watumishi wenye utendaji kazi usioridhisha kwa
mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.” Amesema Mhe.
Simbachawene
Ameagiza nafasi za uongozi zilizowazi katika sehemu za
kazi zijazwe kwa kuzingatia Sheria, Kanuni naTtaratibu zilizopo.
“Tekelezeni jukumu la kuwaandaa watumishi wenu na
mabadiliko mbalimbali yanayoendelea kujitokeza kwa kuwaandalia mafunzo yenye
kukidhi matarajio ya nchi yetu pamoja na mazingira yanayotuzunguka ili
wakabiliane na mabadiliko yanayoendelea kwa kasi duniani.”
Ameongeza
Pia
amewaelekeza Wakuu hao wa Taasisi za Umma kusimamia kwa vitendo, maadili
katika sehemu za kazi za umma ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa siri za
Serikali zinatunzwa vizuri.
“Mnaelekezwa
kuchukua hatua stahiki pale maadili yanapothibitika kuwa yamekiukwa na
Watumishi walio chini yenu.” Amesema Mhe. Simbachawene
Amehimiza uimarishaji wa usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mikataba ya
huduma kwa mteja katika Taasisi na kutoa taarifa za utekelezaji wa mkataba hiyo
kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Pia amewataka kuziba pengo la upungufu wa watumishi
kwa kutoa ajira za mikataba kwa kuzingatia Waraka wa Katibu Mkuu, UTUMISHI kuhusu
kujitolea katika Utumishi wa Umma.
“Utaratibu huu utasaidia kuboresha utoaji wa huduma
kwa wananchi na kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wahitimu wa fani
mbalimbali.”
Mhe. Simbachawene pia amewataka wakuu wa Taasisi za Umma
kutoa nafasi za Mafunzo kwa Vitendo ili kusaidia kuandaa rasilimaliwatu ya
baadaye yenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu ya Serikali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa Wakala za
Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Miji
na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya (hawapo pichani) wakati akifungua kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo jijini
Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Idara za
Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali, Mashirika na
Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Miji na Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri za Wilaya wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Viongozi hao kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo jijini Dodoma.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa maelezo
ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani)
kuzungumza na Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji
Wakuu wa Wakala za Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa
Majiji, Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya
katika kikao kazi cha Viongozi hao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akielezea malengo
ya kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa Wakala za
Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Miji
na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya (hawapo pichani) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo
jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Idara za
Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali, Mashirika na
Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Miji na Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri za Wilaya wakifuatilia
hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati
akifungua kikao kazi cha Viongozi hao kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene (kushoto) akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu wa
Ofisi yake Bw. Xavier Daudi (wa pili kutoka kulia) baada ya Waziri huyo
kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo kwa lengo la kufungua
kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa
Wakala za Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji,
Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya
kilichofanyika jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene (wa kwanza kulia) akielekea kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo
kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji
Wakuu wa Wakala za Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa
Majiji, Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya
kilichofanyika jijini Dodoma. Wengine ni Watendaji wa ofisi hiyo na Viongozi
mbalimbali.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo jijini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Wakuu wa Idara za Serikali zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa
Wakala za Serikali, Mashirika na Taasisi za Umma, Wakurugenzi wa Majiji,
Manispaa na Miji na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya baada ya kufungua kikao
kazi cha viongozi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mabeyo jijini
Dodoma.
No comments:
Post a Comment