Saturday, March 29, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE AELEKEZA NAMNA BORA ZAIDI YA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA KIUTUMISHI IKIWEMO BARUA ZA AJIRA MPYA

 

 

Na. Mwandishi Wetu- Dodoma

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi kuhakikisha barua za walioshinda usaili na kupangiwa vituo vya kazi zinatolewa kwenye mikoa husika walikofanyia usaili badala ya kuwalazimu kusafiri hadi jijini Dodoma Sekretarieti ya Ajira kufuata barua hizo.

 

Amesema kitendo cha watumishi hao wapya kupatiwa barua katika mikoa husika kitasaidia kupunguza gharama, usumbufu pamoja na muda wanaoutumia kufika hadi Dodoma.

 

Mhe. Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo jijini Dodoma wakati akizinda Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 

Mhe. Simbachawene amefafanua kuwa unaweza ukakuta mwananchi amefaulu usaili Mkoa wa Kigoma anaifuata barua jijini Dodoma halafu pengine kapangiwa tena Mkoa huo huo wa Kigoma au Lindi.

 

Mhe. Simbachawene amesema hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi, ikiwemo mwananchi mwenyewe pamoja na fedha anazotumia.

 

“Hii si sawa kwani tunawasumbua wanachoka hata kabla ya kuanza kazi, tuwahurumie, barua hizo wachukulie kwenye mikoa walikofanyia usaili, tuwaamini Makatibu Tawala wetu, tunaamini wapo wataalam wenye maadili wa kufanya kazi hiyo, hivyo tuwape  dhamana waifanye, Mhe. Simbachawene amesisitiza.

 

Amesema anatamani kuona kwa mfano mwananchi aliyefanyia usaili katika Mkoa wa Rukwa anaifuata barua yake katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa kisha  anakwenda pengine  Kigoma alikopangiwa kazi na sio kwenda Dodoma kwanza.

Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu, UTUMISHI, kuandaa kituo cha pamoja (One Stop Centre) katika ofisi hiyo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma, ikiwa ni ubunifu wa kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo  papo kwa hapo kwa Watumishi wenye changamoto za kiutumishi wanaofika Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

 

Amesema Kituo hicho kinatakiwa kiwe na Maafisa Waandamizi wa kila kada ikiwemo wanasaikolojia nguli watakaohakikisha mtumishi yeyote mwenye changamoto za kitumishi anayefika katika Kituo hicho anapata ufumbuzi wa changamoto yake inayomkabili papo kwa hapo.

 

Amefafanua kuwa, kituo hicho kitakuwa na mawasiliano ya waajiriwa wote nchini hivyo mtumishi hatalazimika kurudi tena mkoani kwake kurekebisha taarifa zake badala yake suluhu zote za changamoto alizo nazo  zitapatikana hapo.

 

Amesema hali hiyo itapunguza msururu wa Watumishi wanaotoka maeneo mbalimbali nchini ambapo kila mmoja akifika Ofisini hapo  anataka kumuona na Waziri au Katibu Mkuu.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Simbachawene kwa maelekezo aliyoyatoa na kwa ubunifu huo huku akimuahidi kuyatekeleza kikamilifu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene kuzindua Baraza hilo.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Katibu Mstaafu wa Baraza la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Rocky Setembo akitoa neno la shukrani baada ya kumaliza muda wake katika kulitumikia Baraza hilo kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa TUGHE Mkoa, Bw. Nsubisi Mwasandende.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora mara baada ya kuzindua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora mara baada ya kuzindua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja Viongozi wapya akiwemo Katibu wa Baraza la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Mwendesha Mkandya na Katibu Msaidizi, Bi. Catherine Massawe (kulia waliosimama) mara baada ya kuzindua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.


No comments:

Post a Comment