Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Serikali itaunda timu
ya wataalam itakayojuisha Wizara tano (5) ili kuchambua Makala ya “Non-Employed
Teachers Organisation-NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya kijamii ili maoni
yao yatumike kwa maendeleo ya taifa.
Waziri Simbachawene amesema hayo leo wakati wa kikao
kilichoshirikisha Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia na Viongozi wa NETO kilichofanyika Mtumba jijini
Dodoma.
“Ninamuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw.
Juma Mkomi kuunda timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia na Wizara ya Fedha ili kuchambua makala hiyo ili tuweze kutumia
mapendekezo yao kupata suluhu ya upungufu wa ajira kwa walimu” alisema Mhe.
Simbachawene.
Aidha, Mhe. Simbachawene amesema Serikali ina haki ya
kumsikiliza kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 na kwa kuzingatia misingi ya 4R ya Rais Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Mhe. Simbachawene amesema kuwa Serikali ya Awamu ya
Sita inazingatia misingi ya Falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko
na Kujenga Upya), hivyo ujio wa viongozi na NETO na utayari wa viongozi wa
Serikali kuwasikiliza viongozi hao ni jitihada madhubuti zinazosadifu
uzingatiaji wa falsafa hiyo.
Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.
Prof. Adolf Mkenda amesisitiza kuwa utaratibu wa usaili unaleta ushindani, haki
na kuondoa mwanya wa upendeleo kwa wasailiwa.
“Mapendekezo yenu ni mazuri na sisi kama Serikali tunasubiri
timu iliyotajwa na Mhe. Simbachawene ifanye kazi ya kupitia na kuchambua Makala
hiyo na kisha kuleta ushauri wa namna bora ya kuboresha mchakato wa ajira za
walimu” alisema Mhe. Mkenda.
Vilevile, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi amesema Ofisi yake iko tayari kuunda timu hiyo na itatoa taarifa ndani ya kipindi cha siku 30 hadi 45 zilizoelekezwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao kilichoshirikisha Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu na Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma.
Viongozi wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza kwenye kikao kilichoshirikisha Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu na Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Kaibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Bw. Atupele Mwambene.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.
Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mhe.
Deus Sangu (katikati) na Naibu Kaibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Bw. Atupele Mwambene wakifuatilia kikao
kilichoshirikisha ofisi hizo na Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) kilichofanyika
Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe wa Chama cha Walimu Wasio na Ajira (NETO)
wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza kwenye kikao kilichoshirikisha
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia na Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) kilichofanyika Mtumba
jijini Dodoma.
Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi
ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakifuatilia kikao
kilichoshirikisha ofisi hizo na Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) kilichofanyika
Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiagana na Viongozi na Wajumbe
wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) baada ya kumaliza kikao kilichofanyika
Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi na Wajumbe wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) baada ya
kumaliza kikao kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na
Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi na Wajumbe wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO) baada ya
kumaliza kikao kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma. Wengine ni Viongozi na
Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia.
No comments:
Post a Comment