HABARI KATIKA PICHA:
OFISI YA RAIS-UTUMISHI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2025 KATIKA VIWANJA VYA SHEIKH AMRI ABEID KARUME JIJINI ARUSHA KUANZIA TAREHE 01-8 MACHI, 2025
Baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakitazama bango la Mwongozo
wa Mavazi kwa Utumishi wa Umma wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya
Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha.
Afisa Sheria, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Richard
Lugomela (wa kwanza kulia) akiwahudumia Watumishi wa Umma Wastaafu
waliotembelea banda la Ofisi hiyo kwa lengo la kufuatilia taarifa zao za
kustaafu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yanayofanyika
katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha.
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimpatia vitabu
vya Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma mwananchi aliyetembelea
banda la Ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025
yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha.
Wananchi mbalimbali wakipatiwa taarifa za Kiutumishi
kutoka kwa Maafisa wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume jijini
Arusha.
No comments:
Post a Comment