Na.Lusungu Helela-KILIMANJARO
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema utashi wa kisiasa wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umeiwezesha TAKUKURU kupata vitendea kazi na kutimiza majukumu yake kwenye mazingira wezeshi.
Amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita zaidi ya Watumishi 1000 wameajiriwa na TAKUKURU, ikiwa ni jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuiwezesha TAKUKURU.
Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la TAKUKURU, Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Kamati hiyo kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora.
Amesema mbali na magari 88 TAKUKURU iliyowezeshwa, inatarajia kwa mara nyingine tena kupokea jumla magari 100 ili kuwasaidia maafisa hao kutekeleza majukumu yao mahali popote na saa yeyote wanakohitajika.
Amesema hiyo ni nia ya dhati ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha TAKUKURU inakuwa na vitendea kazi vya kutosha na vya kisasa.
"Taasisi yetu sio tu inaziangalia Taasisi nyingine bali imekuwa mfano na kioo kwa Taasisi nyingine katika kuonesha thamani halisi ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa jengo hili la Rombo" Mhe. Sangu amefafanua.
Katika hatua nyingine Mhe.Sangu ametoa pongezi kwa Kamati hiyo kwani ndiyo imekuwa ikifanya mambo yatokee, " mmekuwa mkipaza sauti kwa kufanya mapendekezo ya marekebisho ya bajeti kwenye miradi ya maendeleo kwenye Taasisi yetu ya TAKUKURU"
Amefafanua kuwa mwaka jana bajeti ya TAKUKURU ilikuwa Sh. Bilion 4.5 ambayo Kamati hiyo iliwatupigania na mwaka huu wa fedha imekuwa Sh. Bil. 6, "Bila kelele ya Kamati yako Mhe.Mwenyekiti tusingepata fedha hizi" amesisitiza
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deus Sangu akizungumza mara baada ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kutembelea na kukagua mradi wa
ujenzi wa jengo la TAKUKURU, Wilaya ya Rombo, Mkoani
Kilimanjaro
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila akizungumza kabla Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuanza
kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la TAKUKURU,
Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe.
Dkt. Joseph Mhagama
(katikati) akiwa na Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu wakiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo mara baada ya
kutembelea na kukagua
mradi wa ujenzi wa jengo la TAKUKURU, Wilaya ya
Rombo, Mkoani Kilimanjaro. Wengine ni Viongozi na Watumishi wa TAKUKURU
Muonekano
wa jengo la TAKUKURU,
Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro ambapo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria waliptembelea na kukagua mradi wa
ujenzi wa jengo hilo.
No comments:
Post a Comment