Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 26 Machi, 2025.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa kuishirikisha Kamati hiyo na kutoa uelewa mpana kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya kamati yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
“Kamati inatoa pongezi nyingi kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu jambo linalodhihirisha kuwa mnaendana na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Serikali inayotekeleza majukumu yake kikamilifu kwa maendeleo ya nchi.” Mhe. Mhagama amesema.
Mhe Mhagama ameitaka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora pamoja na taasisi zake kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali
ili kuleta tija na manufaa nchini yatakayokidhi mahitaji na viwango
vikubwa katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kutoa ushauri, maoni na miongozo mbalimbali ambayo ofisi yake imekuwa ikiifanyia kazi na kwa asilimia kubwa imeisaidia ofisi hiyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
“Mhe. Mwenyekiti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora inajivunia kusimamiwa na Kamati yako kwani mmekuwa mkitupatia ushauri, maoni na miongozo mbalimbali ambayo yameleta tija kwetu na kutufanya tutekeleze majukumu yetu kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa sana.” Mhe. Simbachawene amesema.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria itapokea taarifa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora pamoja na
taasisi zake kwa siku mbili tarehe 26 na 27 Machi, 2025 kwa lengo la kujadili Utekelezaji wa Mpango
na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi
kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama
akizungumza wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene akiwasilisha
taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti
kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka
wa Fedha 2025/26 kwa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (wa
kwanza kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama wakati kamati hiyo
ilipokuwa ikipokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha
2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Kulia kwake
ni Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka, wa tatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI,
Bw. Xavier Daudi.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo
kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha
2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Shedrack Mziray akitoa
ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa
ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka
wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha
2025/26.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Yahya Massare (aliyevaa shati la bluu) akiwasilisha hoja
kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo
na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti
kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka
wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (mstari wa mbele) wakisikiliza fafanuzi
mbalimbali za hoja zilizotolewa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti
kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka
wa Fedha 2025/26.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo (katikati) akiwasilisha hoja kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga
kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing
Investments (WHI), Arch. Sephania Solomon akijibu hoja ya taasisi
anayoisimamia kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga
kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mapango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.
No comments:
Post a Comment