Na. Veronica Mwafisi-Arusha
Tarehe 08 Machi,
2025
Watumishi Wanawake kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wameshiriki kwa wingi kwenye Maadhimisho ya
Siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2025 jijini Arusha ambapo mgeni rasmi
alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiwezeshwa katika
masuala mbalimbali nchini huongeza chachu ya utendaji kazi kwa kuzingatia usawa
wa kijinsia kwa kushirikiana na wanaume na kuleta maendeleo kwa ustawi wa taifa.
Katika kuadhimisha Siku hiyo, Wanawake wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI walipata fursa ya kishiriki kikamilifu maonesho kuanzia tarehe 01
Machi hadi 08 kwenye Kilele cha Maadhimisho hayo kwa kutoa huduma mbalimbali za
Kiutumishi kwa Watumishi wa Umma na Wananchi.
Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu yamefanyika Kitaifa
Jijini Arusha katika Viwanja vya Amri Abeid Karume yaliyobeba kauli mbiu isemayo
“Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”.
Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa
katika picha ya pamoja nje ya Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume wakati wa
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yaliyofanyika jijini
Arusha leo tarehe 08 Machi, 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa
katika maandamano ya kuingia Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume wakati wa
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yaliyofanyika jijini
Arusha leo tarehe 08 Machi, 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa
katika picha ya pamoja nje ya Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume wakati wa
Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yaliyofanyika jijini
Arusha leo tarehe 08 Machi, 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Watumishi Wanawake wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakiwa katika
picha ya pamoja kwenye Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume wakati wa Kilele
cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2025 yaliyofanyika jijini Arusha leo tarehe 08 Machi, 2025 ambapo mgeni
rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
No comments:
Post a Comment