Na. Mwandishi Wetu
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wameaswa kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto pamoja na matumizi sahihi ya namba ya dharula 114 ili kutunza jengo la ofisi hiyo na kuendelea kutoa huduma kwa wateja wanaofika ofisini hapo bila kuwa na shaka yoyote.
Wito huo umetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika wakati wa mafunzo kwa watumishi wa ofisi hiyo yanayotolewa kila Jumatatu ya wiki kwa lengo la kujenga uelewa wa masuala ya kiutumishi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.
Bw. Chanyika ameeleza kuwa, Ofisi ya Rais-UTUMISHI inapokea
wateja wengi kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ili
kulinda usalama wa wateja wanaoingia na kutoka kwa ajili ya kupata huduma hizo ni
muhimu kuchukua tahadhari hasa katika kuangalia usalama wa jengo la ofisi hiyo.
Aidha Bw. Chanyika ameipongeza Ofisi ya Rais-UTUMISHI
kwa kuwa na vifaa mbalimbali vya tahadhari kwa ajili ya kujikinga na madhara ya
moto yanayoweza kutokea.
“Niipongeze ofisi hii kwa kuzingatia usalama wa jengo
kwani nimeona mna vifaa kwa ajili ya tahadhari dhidi ya moto vikiwemo ving’amua
moto,’’ amesema Bw. Chanyika
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji ametoa shukrani kwa niaba ya Watumishi wa
ofisi hiyo kwa mafunzo mazuri ambayo yatasaidia kuongeza umakini katika
utunzaji wa majengo ya ofisi hiyo na kuahidi kuchukua tahadhari zote zinazohusu
kinga dhidi ya majanga ya moto.
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi
Chanyika (kushoto) wakati akielezea namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya
majanga ya moto kwenye mafunzo ya kuwajengea uelewa
watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Bw. Iddi
Chanyika (aliyesimama) akielezea matumizi ya kizima moto cha aina ya unga mkavu
wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu tahadhari dhidi ya majanga ya
moto kwa watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.
Afisa Tawala Mwandamizi,
Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. George Ndatta akifanya zoezi kwa vitendo la kuzima
moto kwa kutumia gesi ya ukaa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa kuhusu tahadhari dhidi ya
majanga ya moto kwa watumishi hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji Bw. Iddi Chanyika (kulia) wakati akifafanua jambo kwenye mafunzo ya uelewa
kuhusu kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas
Ngangaji akitoa shukrani kwa Maafisa
kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara
baada ya kumaliza kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo kuhusu kuchukua
tahadhari dhidi ya majanga ya moto
yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti, Bi. Julieth
Magambo (aliyeinama) akifanya zoezi kwa vitendo la kufungua kizima moto cha
aina ya unga mkavu wakati wa mafunzo
ya kuwajengea uelewa kuhusu tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa watumishi
hao yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma. Anayemwelekeza ni Mkaguzi kutoka Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji Bw. Steven Katte.
No comments:
Post a Comment