Na Mwandishi Wetu - Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza menejimenti ya Ofisi yake kwa kuwa wabunifu katika masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo kubuni tukio la "Utumishi Day Gala”.
Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki hii jijini Dodoma katika Siku maalum ya "Utumishi Day Gala 2025” iliyoandaliwa na menejimenti ya Ofisi yake kwa lengo la kubadilishana uzoefu ili kuboresha utendaji kazi hasa katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itabaki kuwa Ofisi Kiongozi kutokana na bunifu mbalimbali ambazo imekuwa ikifanya kwa lengo la kuhakikisha Watumishi wake wanakuwa vinara wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ameongeza kuwa Ofisi hiyo imekuwa ikijipambanua katika masuala mbalimbali ambayo huwezi kukutana nayo katika Wizara yeyote isipokuwa Utumishi lengo likiwa ni kuhakikisha Watumishi wanajengewa mazingira bora na wezeshi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amesema utamaduni huo wa kukutana mara moja kwa kila mwaka unatoa motisha kwa watumishi na kuongeza ufanisi na uwabikaji katika kutekeleza majukumu yao
Mhe. Simbachawene amesisitiza kuwa ni vema siku hiyo maalum ikatumika kuhamasisha na kuwakumbusha watumishi wa Ofisi hiyo kutimiza wajibu wao kwa kutoa huduma bora kwa wananchi kwani wananchi wakihudumiwa kwa furaha, amani na utumilivu vinatawala nchini.
"Nimebahatika kuwa Waziri katika Wizara tisa lakini huu utamaduni wa kukutana kwa pamoja kama leo hii tulivyokutana hapa tunafurahi kwa pamoja haikuwahi kutokea, hakika hili jambo linapaswa kuigwa na Wizara zingine" alisisitiza Mhe. Simbachawene
Ameongeza kuwa "Unaweza kudhani umeshaona mambo yote kumbe hapana hili la "Utumishi Day Gala" kwangu mimi ni jipya hakika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni Ofisi Kiongozi katika nyanja zote na ndivyo inavyotakiwa, hongereni sana Menejimenti kwa ubunifu huu"
Naye Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Deus Sangu ametumia fursa hiyo kuipongeza timu ya Menejimenti kwa wazo hilo la "Utumishi Day Gala" huku akiwataka Watumishi kufurahia huku wakibadilisha mbinu za kuhakikisha kila mmoja anakuwa kinara wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Awali
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema tukio hilo hufanyika mara moja kila mwaka ambapo Watumishi hukutana
kwa pamoja ikiwa ni fursa adhimu kwao kutokana majukumu mengi
wanayoyatekeleza kuwapelekea kutokuonana kwa pamoja kama ilivyo kwa ''Utumishi Day Gala”
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene akizungumza na watumishi wa ofisi yake kwenye Mji wa Serikali
Mtumba jijini Dodoma katika siku
maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na Menejimenti ya ofisi yake kwa
lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu
akizungumza na watumishi wa ofisi yake jijini Dodoma katika siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025)
iliyoandaliwa na Menejimenti ya ofisi hiyo kwa lengo la kujenga umoja na
kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi yake.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akitoa
neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) kuzungumza na watumishi
wa ofisi hiyo katika
siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa kwa lengo la kujenga umoja
na kuongeza chachu ya utendaji kazi kwa watumishi wa ofisi yake.
Baadhi ya Watumishi wa
Ofisi ya Rais-UTUMISHI waliohudhuria katika siku maalum (UTUMISHI
DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na menejimenti ya ofisi hiyo kwa lengo la kujenga
umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Deus Sangu (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kushoto) katika siku
maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) iliyoandaliwa na menejimenti ya ofisi hiyo jijini
Dodoma kwa lengo la kujenga umoja na kuongeza chachu ya utendaji kazi.
Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George
Simbachawene (wa pili kutoka kushoto) akiwasili katika eneo lililoandaliwa kwa
ajili ya siku maalum (UTUMISHI DAY GALA 2025) kwa lengo la kujenga umoja na
kuongeza chachu ya utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment