Na. Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman amewataka Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (SJMT) na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kuendeleza mashirikiano katika masuala ya utumishi kwa ustawi wa maendeleo ya taifa.
Mhe.
Suleiman amesema hayo leo wakati akihitimisha kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano
katika masuala ya kiutumishi baina ya ofisi hizo mbili
kilichofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
Mhe.
Suleiman amesema kikao hicho kiongeze tija katika utendaji kazi ikiwemo
kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi pamoja na kujadili
changamoto mbalimbali zitakazosaidia kuimarisha utumishi kwa ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya taifa.
Aidha,
Waziri Suleiman amewataka washiriki wa kikao hicho kuwa wazalendo, waaminifu na
waadilifu, kusimamia walio chini yao na kutii maagizo ya viongozi walio juu
yao.
Kwa
Upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akimwakilisha Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. George
Simbachawene amesema kikao hicho kitawajengea uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu yao
ipasavyo kwa kuzingatia miongozo na kanuni za Utumishi wa Umma.
Awali, Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema kikao hicho kitasaidia
kuimarisha mashirikiano mazuri baina ya ofisi hizo mbili na kuahidi kuendelea
kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu kwa masilahi mapana ya
nchi.
Katika
Kikao hicho cha siku tatu moja ya maazimio yaliyopitishwa ni kutoa pongezi kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
kwa kusimamia vema masuala ya Utumishi na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Haroun Ali Suleiman (kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ)
kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kilichofanyika
jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao baina ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman (aliyevaa tai nyeusi) akiwasili katika eneo la kikao kilichofanyika
baina ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika
masuala ya kiutumishi.
Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Afisi
ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi
na Utawala Bora (SMZ) wakiwa
kwenye kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika
masuala ya kiutumishi kilichofanyika
jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi
(aliyesimama) akitoa maelezo ya awali kabla ya kuanza rasmi kwa kikao baina ya ofisi
yake na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ)
kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi
kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi baina ya ofisi hiyo na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman (kulia) akizungumza jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu (katikati) kabla ya Mhe. Suleiman kufunga kikao baina ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI (SJMT) na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.
Viongozi
na Watendaji wa Afisi ya Rais, Katiba,
Sheria, Utumishi na Utawala Bora (SMZ)
wakifuatilia
kikao cha ofisi hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora (SJMT) kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kiutumishi kilichofanyika jijini
Dodoma.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na Viongozi na Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (SJMT) na Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi
na Utawala Bora (SMZ) baada ya kufunga kikao kilicholenga kuimarisha
ushirikiano katika masuala ya kiutumishi.
No comments:
Post a Comment