Na.Lusungu Helela- Dodoma
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeanza kuwanoa Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu kuandaa Daftari la kielektroniki la Huduma za Serikali kwa Taasisi zote za Serikali kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kupata taarifa za huduma zote zinazotolewa na Taasisi za Serikali kwenye chanzo kimoja.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
- UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi wakati akifungua kikao kazi kuhusu Daftari la
Huduma za Serikali kilichowakutanisha baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote
zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,
SACP Mahumi amesema Daftari hilo ni muendelezo wa utengenezaji wa mifumo
ya kuiwezesha serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kufuatia hatua hiyo SACP. Mahumi amewataka Watumishi hao kuzingatia
mafunzo ya uandaaji wa daftari hilo kwani litakuwa chachu ya kuboresha utoaji
wa huduma katika Taasisi za Wizara hiyo.
Amewasihi Watumishi hao kutambua kuwa Mteja ndiyo mlengwa mkuu wa
daftari hilo hivyo wahakikishe huduma zote zinazotolewa na Taasisi zao zinaainishwa na kuingizwa kwenye daftari hilo kwa usahihi wa hali ya
juu.
Akitolea mfano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) SACP. Mahumi
amesema ili Mwananchi aweze kupata huduma katika taasisi hiyo ni lazima awe na
taarifa za kutosha kwa kuzingatia huduma
zinazotolewa, gharama na muda
utakaotumika kupata huduma hizo.
Katika hatua nyingine, SACP. Mahumi amewataka washiriki wa mafunzo hayo
wakawe mabalozi na wakatumie muda kuwafundisha watumishi wengine ili waweze
kujua umuhimu wa daftari hilo.
Awali, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Patrick Marcelline, ameushukuru
uongozi wa Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa
mafunzo hayo muhimu, na kuahidi kuwa Wizara itayatumia Mafunzo hayo kama nyenzo
muhimu ya kuboresha huduma zake kwa maslahi mapana ya Uhifadhi na Utalii na
Taifa kwa ujumla
Kikao kazi hicho cha siku tatu cha uandaaji wa Daftari la Huduma za
Serikali kinawezeshwa na timu ya wataalam wabobezi kutoka Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP.Ibrahim Mahumi akizungumza wakati akifungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali kilichowakutanisha baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP.Ibrahim Mahumi akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Patrick Marcelline mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali kilichowakutanisha baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii
Baadhi ya Watumishi kutoka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi akizungumza wakati akifungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa kutoka
Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Patrick Marcelline akizungumza kabla ya
kumkaribisha Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP. Ibrahim
Mahumi kuzungumza na Watumishi wakati akifungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali
Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, SACP.Ibrahim Mahumi
akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara
ya Maliasili na Utalii mara baada
kufungua kikao kazi kuhusu uandaaji wa Daftari la Huduma za Serikali
No comments:
Post a Comment