Tuesday, February 18, 2025

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA TASAF ZANZIBAR

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika kisiwa cha Unguja Zanzibar.

Kamati hiyo, imetoa pongezi hizo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Ukumbi wa Mitihani na  Dahalia ya wanafunzi wa kike katika skuli ya Sekondari Kizimkazi Dimbani iliyopo mkoa wa Kusini Unguja  iliyojengwa na TASAF.

Dahalia hiyo ya kisasa yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 248, imelenga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa kwa wanafunzi wa skuli ya Kizimkazi Dimbani.

 Akizungumza leo kwa niaba ya Kamati hiyo   mara  baada ya kutembelea mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati  Mhe. Florent Kyombo amesema, ujenzi wa dahalia hiyo ni kielelezo na   unasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma  za kijamii pamoja kwa wanachi wa shehia ya Kizimkazi Dimbani .

“Tunaipongeza TASAF kwa kazi nzuri iliyofanyika hapa, tumejionea mradi huu ulivyotekelezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu,  miradi ya aina hii ni muhimu sana kwani inachochea ari  ya kusoma kwa wanafunzi wetu,” asisitiza

 “Tumeona ni miradi inayoleta tija na imetekelezwa kwa ubora na thamani ya fedha imeonekana, hii ni kazi nzuri ambayo Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kuifanya kupitia TASAF lakini pia usimamizi mzuri ulipofanywa na Rais Mhe Dkt Hussein Mwinyi kupitia  ofisi zinazosimamia TASAF visiwani Zanzibar" 

 Kwa upande wake, Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu, amesema utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Miundombinu ya utoaji huduma za kijamii unaofanywa na TASAF unalenga kusogeza huduma za kijamii karibu na wanachi  pamoja na kuboresha huduma hizo.

 “TASAF imeweza kujenga shule, madarasa, vituo vya afya, zahanati, madaraja, barabara pamoja na miundombinu ya maji na umwagiliaji, hii yote ni kutaka  kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii" amesema Mhe.Sangu 

Amesema ujenzi huo wa dahalia kwa ajili ya watoto wa kike wapatao 248  uliogharimu kiasi cha Shilingi  Milioni 336 utakuwa mkombozi kwa watoto hao kwa kuwa karibu na shule hali itakayosababisha mahudhurio na ufaulu kuwa mzuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo. 

 Mbali na hilo, Mhe.Sangu amesema Kamati imejionea na imeridhika na  thamani halisi ya fedha ya ujenzi wa bwalo kwa ajili ya chakula kwa ajili ya watoto hao kike katika shule na hivyo kuwafanya watoto hao kusoma shule katika mazingira mazuri na rafiki kwa ajili ya mustakabali ya maisha yao ya badae.

 Awali Mwakilishi wa  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TASAF,  Bw. Godwin Mkisi alisema utekelezaji wa miradi  unalengo la kuboresha huduma za kijamii na katika  maeneo yote ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Alisema, Katika kipindi cha Pili cha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, jumla ya miradi 14 ya miundombinu ya elimu na afya yenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 imetekelezwa hadi kufikia mwezi Januari 2025. Kati ya miradi yote hiyo miradi 11 imekamilika na kukabidhiwa sekta husika na miradi mitatu bado inaendelea na utekelezaji

 

 


Moja ya dahalia  ya kisasa yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 248 ambayo  imelenga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa kwa wanafunzi wa skuli ya Kizimkazi Dimbani iliyojengwa kupitia  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika kisiwa cha Unguja Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,   Mhe. Florent Kyombo akizungumza na Wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika kisiwa cha Unguja Zanzibar. 
Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu akiwa ameongoza na baadhi ya Wajumbe wa ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiangalia mabomba ya maji katika dahalia
Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu akiwa ameongoza na baadhi ya Wajumbe wa ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakikagua baadhi ya vitanda vya watoto wa kike katika moja ya chumba katika  dahalia iliyojengwa kwa ufadhili wa Mradi wa TASAF 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe, Hamza Hassan Juma akiwa kwenye picha ya pamoja na   Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu mara baada ya kufanya mazungumzo wakati Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuanza  kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia TASAF, Wengine ni viongozi wa TASAF Zanzibar 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe, Hamza Hassan Juma akizungumza na    Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu mara kabla ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia TASAF
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,   Mhe. Florent Kyombo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  mara baada ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya  kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika kisiwa cha Unguja Zanzibar
  Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu  wakati akizungumza na wanufaika  wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)  mara baaada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi iliyotekelezwa na  TASAF
Baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsikiliza   Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Mhe. Deus Sangu  wakati akizungumza nao mara baaada ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi iliyotekelezwa na  TASAF

No comments:

Post a Comment