Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya mkutano wa kujadili amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
Mhe. Kagame amewasili asubuhi ya leo Jumamosi Februari 8, 2025 na kupokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Mkutano huo unafanyika huku vikundi vya waasi chini ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23) vimekamata miji ya Goma, Kivu Kaskazini na Nyabibwe, Kivu Kusini vikielekea Bukavu.
Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya mkutano wa kujadili amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya mkutano wa kujadili amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
No comments:
Post a Comment