Na Lusungu Helela- ARUSHA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imefanikiwa kujenga mfumo ambao unawezesha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini kuunganishwa, kuwasiliana na kubadilishana taarifa.
Amesema kwa sasa mifumo 218 kutoka kwenye Taasisi zipatazo 181 imeunganishwa na inasomana.
Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kuitikia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutaka mifumo inayotumika kwenye Taasisi za Umma kusomana ili kurahisisha utendaji kazi Serikalini na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo Februari 11, 2025 jijini Arusha wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Mpango akifungua Kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Amesema e-GA itaendelea kusimamia uunganishwaji wa mifumo ya kubadilishana taarifa kulingana na mahitaji yaliyopo.
Aidha, Mhe. Simbachawene amesema kikao kazi hicho kilimualika Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kumshukuru kwa mchango wake mkubwa pamoja na kutoa hamasa katika matumizi ya TEHAMA kwani ndiyo chachu iliyopelekea mafanikio hayo yanayoonekana kitaifa na kimataifa.
Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amesema Tanzania imeweza kutambulika Duniani kwa kushika nafasi ya pili katika Bara la Afrika na kuwa ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye ripoti ya utafiti wa ukomavu wa matumizi ya teknolojia katika kutoa huduma za Serikali na ushirikishwaji wa wananchi kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia.
Ameongeza kuwa “Kama nchi tumepiga hatua kubwa katika uwezo wa kujenga miundombinu ya kuhifadhi taarifa na kuweza kubadilisha utendaji kazi wetu kwenda kwa njia ya mtandao"
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, ( e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba alisema e-Ga imesaidia matumizi sahihi na ya uhakika kwenye Taasisi za Serikali kwa kuwezesha utoaji wa huduma kwa wakati.
Amesema e-GA imeleta mapinduzi makubwa katika matumizi ya TEHAMA Serikalini kwani imechagiza utendaji kazi wa Serikali na kuongeza ufanisi kwenye Taasisi mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ( NIDA) Mifumo ya fedha ya Benki Kuu ( BOT) pamoja na Mfumo wa Manunuzi ( Nest)
Naye Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka amesema e-GA imeleta mageuzi makubwa kwenye Taasisi za Serikali kwa kuboresha utendaji kazi wa kila siku na utoaji wa huduma kwa jamii kuwa rahisi na wa haraka
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama amesema Bunge ni moja ya wanufaika wakubwa wa gunduzi zilizofanywa na e-Ga.
Amesema Serikali imepiga hatua kubwa kwenye matumizi ya mifumo ya TEHAMA ambayo yameleta tija na ufanisi wa hali ya juu latika utoaji wa huduma bora za haraka na za uhakika kwa wananchi.
"Tunaipongeza sana e-GA kwa bunifu wanazoendelea kufanya, kama Bunge tunataka mifumo yote ya kidigitali inayotumika na Serikali isimamiwe na idhibitiwe na e-GA ili kulinda taarifa za Serikali.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza
kwa niaba ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao
kinachofanyika kwa muda wa siku tatu jijini Arusha
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
George Simbachawene akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuzungumza kwa niaba ya Rais
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha
5 cha Serikali Mtandao kinachofanyika kwa muda wa siku tatu jijini Arusha
Sehemu ya Washiriki wa kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kinachofanyika kwa muda wa siku tatu jijini Arusha kilichofunguliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Mpango akiwa
ameongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ufunguzi wa Kikao
kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kinachofanyika kwa muda wa siku tatu jijini
Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kinachofanyika kwa muda wa siku tatu jijini Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuzungumza kwa niaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kinachofanyika kwa muda wa siku tatu jijini Arusha
No comments:
Post a Comment