Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wametakiwa kuzingatia na kubadili mfumo wa maisha ili kujiepusha na maradhi yasiyoambukiza kwa lengo la kuwahudumia wananchi pasipokuwa na changamoto zozote za kiafya.
Wito
huo umetolewa leo February 24, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge
wakati akiwasilisha mada kuhusu afya kwenye mafunzo
ya kuwajengea uwezo watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Dkt. Kisenge amesema Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu
yanatokana na namna
watu wanavyoendesha maisha yao hivyo, ni vema kupunguza matumizi makubwa ya sukari na matumizi ya ulaji wa chumvi nyingi inayosababisha
shinikizo la juu la damu ambalo moja ya madhara yake ni kutanuka kwa moyo ambao matibabu yake ni gharama kubwa.
Aidha, Dkt. Kisenge amewataka
watumishi wa ofisi hiyo kujitahidi kutumia mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na
kuzingatia lishe bora ili kukabiliana na
magonjwa ya moyo.
Dkt. Kisenge ametoa wito kwa watumishi
hao kupima afya zao mara kwa mara ili kujua tatizo mapema pamoja na kupunguza
gharama za matibabu kwani ugonjwa ukishakuwa mkubwa gharama huongezeka zaidi.
Akihitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi
hao, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amemshukuru Dkt. Kisenge
pamoja na wataalamu alioambatana nao kwa kutoa elimu hiyo kwa watumishi wa
ofisi yake na kuahidi kuzingatia suala la afya ili kutoa huduma bora kwa
wananchi kwa ustawi wa Taifa la Tanzania.
Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na
Ofisi ya Rais –UTUMISHI wa kutoa uelewa kuhusu masuala mbalimbali katika
Utumishi wa Umma ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akisisitiza jambo wakati
wa mafunzo kuhusu utunzaji wa afya bora yaliyofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba,
jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi
wa ofisi yake.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo kuhusu utunzaji wa afya
yaliyofanyika katika ofisi
hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama)
akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa mafunzo kuhusu utunzaji wa
afya bora yaliyofanyika
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akifanya
wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa
watumishi wa ofisi hiyo
katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji
kazi.
Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (katikati) akifuatilia wasilisho kuhusu Magonjwa
ya Kisukari na Shinikizo la damu
wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika
Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na
kuimarisha utendaji kazi.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo kuhusu utunzaji wa afya
bora yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mafunzo kuhusu utunzaji wa afya
bora yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa
Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala
Bora, Bw. Stephano Mgala (aliyenyanyua
mkono) akiuliza swali kuhusu afya
mara baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge
(hayupo pichani) kuwasilishwa mada kuhusu
Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu
wakati wa mafunzo yanayotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika
Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na
kuimarisha utendaji kazi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (wa kwanza kushoto)
akifuatilia wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu
wakati wa mafunzo yanayotolewa kwa watumishi wa ofisi hiyo katika
Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na
kuimarisha utendaji kazi. Wa tatu kutoka kushoto
ni Naibu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge
(hayupo pichani) wakati akifanya wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu
kwenye mafunzo yaliyofanyika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la
kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya
Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge
(hayupo pichani) wakati akifanya wasilisho kuhusu Magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la damu kwenye mafunzo yaliyofanyika
Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi.
No comments:
Post a Comment