Friday, February 1, 2019

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WA TAARIFA KATIKA UTEKELEZAJI WA SERIKALI MTANDAO

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifungua rasmi kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichowajumuisha Watendaji Wakuu Serikalini katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Taasisi serikalini wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akiwakaribisha katika mkoa wake wajumbe wa kikao kazi cha pili cha  Serikali Mtandao kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao, Dkt. Jabiri Bakari akizungumza kabla ya ufunguzi wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge wakati wa kikao kazi cha pili cha Serikali Mtandao katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu Dodoma.

No comments:

Post a Comment