Friday, February 15, 2019

DKT. MWANJELWA AWATAKA WANUFAIKA WA TASAF WILAYANI PANGANI KUTUMIA FEDHA ZA RUZUKU WANAZOZIPATA KUBORESHA MAISHA YAO KIUCHUMI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, alipowatembelea wanufaika hao wilayani humo kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo na kupata shuhuda za walengwa. 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said wakiwa nyumbani kwa mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilaya ya Pangani, mara baada ya kuitembelea familia ya  mnufaika huyo ili kushuhudia namna fedha za ruzuku zilivyomnufaisha mlengwa huyo.

Baadhi ya wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipowatembelea wanufaika hao kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo na kupata shuhuda za walengwa. 


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said wakifurahia jambo na mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani (kushoto) nyumbani kwa mmnufaika huyo mara baada ya kumtembelea na kushuhudia cherehani aliyoinunua pamoja na nyumba aliyoijenga kutokana na fedha za ruzuku anazozipata.


No comments:

Post a Comment