Sunday, February 24, 2019

MHE.MKUCHIKA APONGEZA WANUFAIKA WA TASAF WA KIJIJI CHA MKWANYULE WILAYANI KILWA KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akizungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), kuzungumza na wanufaika wa TASAF wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.

Wakazi wa kijiji cha Mkwanyule wilayani Kilwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) katika mkutano wa Waziri huyo na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa.

Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara akiishukuru serikali kwa kuufikisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani kwake wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani humo.

Mmoja wa wanufaika wa TASAF mkazi wa kijiji cha Mkwanyule Bi. Mwanahamisi Ally Ukwenda akishuhudia namna alivyonufaika na TASAF wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa. Kushoto kwake ni mnufaika mwenzie Bi. Atili Masoud Swalehe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (kulia) akikagua mradi wa mbuzi unaomilikiwa na Bw. Hassan Charahani (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano kati yake na wanufaika wa TASAF uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mkwanyule wilayani Kilwa.

No comments:

Post a Comment