Thursday, February 21, 2019

MHE. MKUCHIKA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Sarah Chiwamba na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule.

Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Bi. Luiza Mlelwa, akiwasilisha taarifa ya halmashauri yake wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri hiyo mkoani Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Sarah Chiwamba akitoa utambulisho wa wageni waliohudhuria kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kilichofanyika katika viwanja vya halmashauri hiyo mkoani Lindi.

No comments:

Post a Comment