Friday, February 1, 2019

SERIKALI YAELEKEZA KUSIMAMISHWA KAZI MKUU WA IDARA YA UTAWALA NA UTUMISHI WA MANISPAA YA ILALA NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU WATUMISHI WENGINE WA MANISPAA HIYO



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wanaohusika na Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akifafanua kuhusu kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Manispaa ya Ilala Bi. Benadeta Mwaikambo wakati akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ofisini kwake jijini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi na Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bi. Aneth Andrew.



No comments:

Post a Comment