Thursday, February 7, 2019

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WAKE



Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga akihimiza uzingatiaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa Umma  nchini mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa sehemu ya mapokezi kusaini kitabu cha mahudhurio wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanywa na Idara ya Ukuzaji  Maadili, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo na kuwahi kazini.

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga  akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uadilifu wa ofisi hiyo wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanyika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo kwa watumishi wa umma nchini.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uadilifu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Constantino L. Kinawiro (mwenye suti) akipongezwa na mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment