Monday, February 25, 2019

MHE.MKUCHIKA ATOA SIKU 34 KWA AFISA UTUMISHI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA KUWEKA TAARIFA SAHIHI ZA WATUMISHI KWENYE MFUMO WA HCMIS



Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule akitoa utambulisho wa makundi ya watumishi waliohudhuria kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.


Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe.Christopher Ngubiagai akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi (hawapo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Christopher Ngubiagai (kulia kwake).


Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa


Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bi. Jovita Buyobe akijibu hoja wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, wilayani Kilwa.

No comments:

Post a Comment