Thursday, February 21, 2019

MHE. MKUCHIKA AWAASA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA KUTUMIA FEDHA ZA TASAF KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA YA KUONDOKANA NA UMASKINI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi (hawapo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Dkt. Bora Haule akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.

Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi. Zainabu Matata akitoa ushuhuda wa namna TASAF ilivyomuwezesha kujenga nyumba na kulipia ada ya mtoto wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF Wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi. Somoe Nchilima akitoa ushuhuda wa namna TASAF ilivyomuwezesha kujiunga na kilimo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na wanufaika wa TASAF Wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Bw. Ahmad Makoroganya akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kutembelea wilayani kwake katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

No comments:

Post a Comment