Tuesday, February 19, 2019

MAOFISA WALIOHUSIKA KUTOAJIRI WATUMISHI SITA BAADA YA KUPEWA KIBALI CHA AJIRA NA KATIBU MKUU UTUMISHI KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KINIDHAMU



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi chenye  lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Kilindi. 

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao,  kabla ya  kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Kilindi. 

Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Mhe. Omary Kigua akiwasilisha hoja za kiutumishi za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi  kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.


No comments:

Post a Comment