Wednesday, June 26, 2019

SERIKALI YAWAASA WANANCHI KUTOTUMIA DAWA ZA KULEVYA ILI KULINDA NGUVUKAZI YA TAIFA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano, jijini Tanga.
 
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano, jijini Tanga.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) akizungumza na wananchi wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano, jijini Tanga. 
Mmojawapo wa waathirika wa dawa za kulevya, Bw. Said Bandawa akitoa ushuhuda wa namna Serikali ilivyomsaidia kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya kupiga vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano, jijini Tanga.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiteta jambo na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya kupiga vita Dawa za Kulevya duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Tangamano, jijini Tanga.

Tuesday, June 25, 2019

WATUNZA KUMBUKUMBU NA MAAFISA RASILIMALIWATU WATAKIWA KUZINGATIA UADILIFU KATIKA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA SERIKALI



Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael kufungua kikao kazi cha siku tatu cha Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini chenye lengo la kujadili masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akifungua kikao kazi cha siku tatu cha Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini chenye lengo la kujadili masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akisisitiza jambo alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku tatu cha Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini chenye lengo la kujadili masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.

Baadhi ya Washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku tatu cha Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini chenye lengo la kujadili masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akiwa katika kikao kazi cha siku tatu cha Watunza Kumbukumbu na Maafisa Rasilimaliwatu Serikalini chenye lengo la kujadili masuala ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka katika Utumishi wa Umma kilichoanza leo jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi

Saturday, June 22, 2019

DKT. MWANJELWA ASHANGAZWA NA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO KUTOA KIWANJA KWA WAJASIRIAMALI KATIKA ENEO HATARISHI



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Dkt. Kebwe Steven Kebwe alipomtembelea ofisini kwake kabla kuanza ziara ya kikazi ya kukagua vikundi vya wajasiriamali waliorasimishwa katika Manispaa ya Morogoro.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Mwenyekiti wa kikundi cha usindikaji wa vyakula na viungo, Bi. Emmy Kiula wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua vikundi vya wajasiriamali waliorasimishwa katika Manispaa ya Morogoro.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Mwenyekiti wa kikundi cha utengenezaji wa milango na madirisha ya chuma, Bw. Abdallah Chunga alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua vikundi vya wajasiriamali waliorasimishwa katika Manispaa ya Morogoro.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitoa maagizo kwa watendaji wa MKURABITA na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro alipokuwa akihitimisha ziara yake ya kikazi ya kukagua vikundi vya wajasiriamali waliorasimishwa katika Manispaa ya Morogoro.