Monday, March 2, 2026

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDHIBITI VVU/UKIMWI NA MSY WASISITIZWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU

 Na. Antonia Mbwambo - Kagera

Tarehe: 2 Machi, 2026

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Leila Mavika amewaelekeza Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa na waratibu ngazi ya Wizara, Taasisi zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kujenga Utumishi wa Umma wenye afya, tija na unaoendana na matarajio ya wananchi.

Bi. Mavika ameyasema hayo  leo tarehe 02 Machi, 2026  wakati akifungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa.

Aidha Bi. Mavika amezipongeza Taasisi za Umma ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika kusimamia afua za VVU, UKIMWI na MSY hasa kwenye Kuratibu kampeni za upimaji wa hiari wa VVU na utoaji wa elimu ya lishe bora, mazoezi na afya ya akili.

“Haya mafanikio ni ya kujivunia, lakini bado tunayo safari ya kwenda kufikia malengo tuliyojiwekea pamoja na mafanikio hayo” Bi. Mavika alisema.

Vilevile Bi. Mavika amesisitiza kuwa ushirikiano wa Wadau na Taasisi simamizi za Kudhibiti VVU UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza ikiwemo Wizara ya Afya, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), na wadau wengine ni muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa afua hizo unaendana na miongozo ya kitaifa.

Amehitimisha kwa kuwataka Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa na waratibu kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kuweka vipaumbele vinavyoendana na hali halisi ya watumishi na kuhakikisha kuwa kila taasisi ina mpango kazi unaotekelezeka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo amemshukuru Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa utayari wake katika utekelezaji wa majukumu yaliyokasimiwa katika kuimarisha afya na ustawi wa Taifa.

Naye Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Bwai Biseko akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, amewashukuru waratibu   kwa namna ambavyo wameshiriki kikamilifu katika kikao hicho na kutoa wito kwa kila mshiriki kuzingatia na kutekeleza yote yaliyoshauriwa.

 

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi hiyo Bi. Leila Mavika akitoa hotuba ya Mgeni Rasmi katika kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera

Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa utayari wake katika utekelezaji wa majukumu yaliyokasimiwa katika kuimarisha afya na ustawi wa Taifa wakati wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera

Washiriki wa Kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya kitaifa ya kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza baada ya Mgeni Rasmi kufungua kikao cha Afua kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera

Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mhe. Bwai Biseko akitoa neno la Utangulizi kabla ya kumkaribisha mwakilishi wa Katibu Mkuu-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika katika Ufunguzi wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa kilichofanyika leo tarehe 2 Machi, 2026 katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera.

Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Leila Mavika (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, wa Ofisi hiyo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti magonjwa hayo ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa    kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera.

Mratibu wa Mkoa wa Kagera Bw. Amosi Adonias akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Muongozo wa kudhibiti VVU/UKIMWI katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za magonjwa hayo katika  kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera leo tarehe 2 Machi, 2026.

Mratibu wa Mkoa wa Kagera Bw. Amosi Adonias akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Muongozo wa kudhibiti VVU/UKIMWI katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za magonjwa hayo katika  kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera leo tarehe 2 Machi, 2026.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Leila Mavika (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu wa Kamati ya kitaifa pamoja na wajumbe ngazi ya Wizara na Mkoa baada ya kufungua Kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa wakati wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti magonjwa hayo ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa    kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera.

Afisa Ustawi wa jamii Mwandamizi Bi. Juliana Ntukey akiwasilisha mada kuhusu Mwongozo na Waraka wa kudhibiti VVU, UKIMWI na MSY 2014 wakati wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti magonjwa hayo ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa    kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera.

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania Dr. Hafidh Ameir akitoa wasilisho kuhusu wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa wakati wa kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti magonjwa hayo ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa    kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Bi. Leila Mavika akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa lengo la kufungua kikao kazi cha
kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa kilichofanyika mkoani hapo leo tarehe 2 Machi, 2026


Washiriki wa Kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza ya kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2025/2026 ngazi ya Mkoa na Taifa wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya kitaifa ya kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa Sugu Yasiyoambukiza baada ya Mgeni Rasmi kufungua kikao cha Afua kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT Bukoba Mkoani Kagera