Friday, January 30, 2026

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEKELEZA AHADI YA RAIS YA KUAJIRI VIJANA NDANI YA SIKU 100

 Na. Antonia Mbwambo, na Veronica Mwafisi- Dodoma

 Tarehe: 30 Januari, 2026

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali kupitia Ofisi yake imetekeleza ahadi ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuajiri vijana 12,000 ndani ya siku 100 za kwanza za kipindi cha pili cha awamu ya sita.

Waziri Kikwete amesema hayo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Januari 30, 2026 katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma.

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi kuajiri vijana 5,000 kwa sekta ya Afya na watumishi 7,000 kwa sekta ya elimu ambao ni Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati.

Mhe, Kikwete alisema kuwa hadi tarehe 20 Januari, 2026 watumishi hao wapya wamepatikana na wamepangiwa vituo na barua za ajira zimetumwa moja kwa moja kwenye akaunti za waombaji hao na wamesharipoti katika vituo vyao vya kazi.

“Kwa sasa mambo yote yanakwenda kidijiti ambapo watumishi hao wapya wamepokea barua zao za ajira kwa njia ya simu za mkononi na wameripoti kwenye vituo vyao vya kazi na waliowahi kabla ya kutuma taarifa za mishahara wamepokea mshahara wao wa kwanza mwezi huu wa Januari” Mhe. Kikwete aliongeza.

Aidha Mhe. Kikwete ametoa wito kwa waajiriwa wapya ambao bado hawajaripoti katika vituo walivyopangiwa kufanya hivyo ndani ya siku 14 tangu walipopokea barua ya kazi, kinyume na hapo nafasi zao zitachukuliwa na wasailiwa wengine ambao wapo katika kanzi data.

Mh. Kikwete ametoa wito kwa Vijana wa kitanzania kuwa kwa wale wote wenye sifa wasisite kuomba nafasi za ajira pindi zitakapotangazwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwani Serikali bado itaendelea kutangaza nafasi hizo.

Kadhalika Mhe. Kikwete amesema, katika kutekeleza ahadi za siku 100 za Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, Ofisi ya Rais, Menejiementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeboresha Mfumo wa kielektroniki wa e-Mrejesho ambapo Wananchi wanaweza kuwasilisha maoni au malalamiko kupitia mfumo huo ili kuimarisha Utawala Bora.

Mhe. Kikwete amehitimisha kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kutoa maelekezo ya kuhakikisha vijana wanapata ajira ili kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.

 

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama makala maalum kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Katikati ni Naibu Waziri wake Mhe. Regina Qwaray na wakwanza kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa kwanza kulia) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.

Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Uhuru, Bw. Fred Alfred (aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kuhusu ajira wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (wakwanza mstari wa mbele kulia) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Wengine ni Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora. 

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.

 

Tuesday, January 27, 2026

KIKWETE AITAKA BODI YA USHAURI KUISIMAMIA VYEMA MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahia jambo wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) katika ukumbi wa mikutano wa e-GA Mtumba - Jijini Dodoma, Januari 27,2026.


Na: Mwandishi Wetu, Dodoma

Tarehe 27 Januari, 2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amezindua bodi ya ushauri ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kuitaka ihakikishe inaisimamia Mamlaka hiyo vyema na kutoa ushirikiano kwa menejimenti katika utatuzi wa changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yake.

Mhe. Kikwete ametoa wito huo  leo Januari 27,2026.alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya e-GA katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo iliyopo Mtumba - Jijini Dodoma.

Mhe. Kikwete amempongeza Dkt. Mussa Kissaka kwa kuteuliwa na Rais kwa mara ya pili kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na kumhakikishia ushirikiano wa dhati ili kutimiza malengo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa Serikali Mtadao yenye tija.

“Ninafahamu Mamlaka imekuwa ikipata changamoto katika utekelezaji wa majukumu yake hasa pale taasisi zinaposhindwa kutekeleza sheria, kanuni, viwango na miongozo ya serikali mtandao, hivyo wekeni mikakati bora ya kudhibiti jambo hilo” alisisitiza Mhe. Kikwete.

Aidha, aliongeza kuwa moja ya mambo ambayo watumishi wa umma bado wanakiuka kwa makusudi au kwa kutofahamu ni suala la kutumia anuani za baruapepe ambazo sio za Serikali katika kutuma au kupokea taarifa za kiofisi jambo ambalo linasababisha kuvuja kwa siri za Serikali.

Pia, alisisitiza kuwa kila Wizara, Idara zinazojitegemea, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kutumia anuani za baruapepe za Kiserikali zilizo kwenye utaratibu wa  .go.tz, .gov, au .org katika kutuma au kupokea taarifa za kiofisi kwa njia ya baruapepe vinginevyo Sheria ichukue mkondo wake.

Vile vile, Mhe. Kikwete ametumia fursa hiyo kumtakia kila la kheri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku hii ya kuzaliwa kwake. Aidha, amemuombea dua kwa Mwenyezi Mungu ili amjalie Rais kheri, afya njema na umri mrefu ili aone wananchi wanavyonufaika na yale aliyoyaanzisha na kuyatekeleza kwa manufaa ya taifa.

Mhe. Kikwete amepanda mti wa muembe ikiwa ni ishara ya kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Mti huo umepandwa katika eneo la Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mtumba- Dodoma, tarehe 27 Januari, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya e-GA mara baada ya uzinduzi rasmi wa bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa e-GA Mtumba - Dodoma, Januari 27,2026.

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya eGA na Menejimenti wakufuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Ushauri, Mtumba Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Kushoto) akiwasili katika Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA)  kwa kazi ya kuzindua Bodi ya Ushauri na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo zilizopo Mtumba- Dodoma, tarehe 27 Januari, 2026. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa eGA Eng. Benedict Ndomba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya e-GA Dr. Mussa Kissaka akipanda mti wa kumbukumbu baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akipanda mti wa muembe ikiwa ni ishara ya kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Mti huo umepandwa katika eneo la Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mtumba- Dodoma, tarehe 27 Januari, 2026. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa eGA Eng. Benedict Ndomba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akipanda mti wa muembe ikiwa ni ishara ya kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Mti huo umepandwa katika eneo la Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mtumba- Dodoma, tarehe 27 Januari, 2026. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa eGA Eng. Benedict Ndomba.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya e-GA Dr. Jasmine Tiisekwa akipanda mti wa kumbukumbu baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete (Kulia) akielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) inayojengwa Mtumba, Dodoma.  Kushoto ni Mkurugenzi wa e-GA Eng. Benedict Ndomba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akipanda mti wa muembe ikiwa ni ishara ya kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Mti huo umepandwa katika eneo la Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mtumba- Dodoma, tarehe 27 Januari, 2026. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa eGA Eng. Benedict Ndomba.


HERI YA SIKU YA KUZALIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

 


KUELEKEA 27 YA KIJANI

 





Monday, January 26, 2026

PONGEZI YA KUZALIWA MWEZI JANUARI KWA WATUMISHI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATOLEWA

 Watumishi wote wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI waliozaliwa Mwezi Januari wamepongezwa leo tarehe 26 Januari, 2026.

Kwa kumbukizi hiyo, watumishi hao wamepata nafasi ya kulishwa Keki na Mkurugenzi wa Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu Bi. Mariam Mwanilwa kwa niaba ya Katibu Mkuu Bw. Juma Mkomi.















AJIRA MPYA 980 TAKUKURU KUONGEZA NGUVU KATIKA MAPAMBANO YA RUSHWA NCHINI-Mhe. Kikwete

 Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi-Morogoro

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ajira mpya 980 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zitaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Mhe. Kikwete amesema hayo wakati akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuzungumza na Viongozi wa TAKUKURU na Wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Cate mkoani Morogoro.

Amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa kibali cha ajira hizo na kuwatahadharisha watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa. “Katika kuboresha utendaji kazi wa Utumishi wa Umma nchini hatua kali zitachukuliwa kwa watumishi watakaojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwa na utumishi wa umma unaozingatia Taratibu, Kanuni, Sheria na Miongozo,” amesisitiza.

Mhe. Kikwete ameahidi kuwa, ofisi yake itaendelea kusimamia taasisi ya TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria na kadri ya maelekezo ya Mhe. Rais yatakavyotolewa ili kuongeza tija na kutoa haki stahiki kwa wananchi kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa uwezeshaji mkubwa wa mara kwa mara katika taasisi hiyo ikiwemo rasilimaliwatu, fedha ambazo zimesaidia kujenga majengo mbalimbali ya TAKUKURU na vifaa mbalimbali vya utendaji kazi.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amesema ofisi yake inaendelea na utekelezaji wa shughuli zake kwa mujibu wa Sheria ambapo wamedhamiria kuimarisha kwa vitendo jitihada za Serikali juu ya mapambano dhidi ya rushwa nchini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, Bw. Chalamila amesema, TAKUKURU inaendelea na kazi ya kuelimisha umma mijini na vijijini kuhusu masuala ya rushwa na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kuzuia vitendo vya rushwa kwa manufaa ya nchi.

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU hufanyika kwa lengo la kubainisha changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi wao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja. Mkutano huu una kaulimbiu ya “Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu, tutimize wajibu wetu”.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.

Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika leo tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila 

Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila (kushoto)
akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye (kulia) baada ya kuwasili katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika leo tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza Kushoto) akiwa tayari kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika leo tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye wa TAKUKURU akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Felister Shuli wakati walipokuwa katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika Mkoani Morogoro

Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.

 

Saturday, January 24, 2026

SERIKALI KUIMARISHA UFANISI WA UTENDAJI KAZI KUPITIA UJENZI WA OFISI ZA TAKUKURU

 Na. Veronica Mwafisi na Antonia Mbwambo-Chalinze

Tarehe 24 Januari, 2026

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema uzinduzi wa jengo la TAKUKURU katika Halmashauri ya Chalinze ni hatua muhimu inayothibitisha dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha mazingira ya utendaji kazi, kuongeza ufanisi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuleta Maendeleo ya Watanzania.

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo leo Mkoani Pwani katika Halmashauri ya Chalinze wakati akizindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU ambalo litaboresha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi wa TAKUKURU ikiwemo utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Mhe Kikwete amesema kuwa, Serikali imewawezesha TAKUKURU kwa kiwango kikubwa sana hivyo amewaasa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa bidii na weledi zaidi ili dhamira ya Serikali ya kuitokomeza rushwa nchini pamoja na maono ya TAKUKURU ya kuwa na Tanzania isiyo na rushwa yaweze kufikiwa.

Vilevile, Mhe. Kikwete ametoa wito kwa Watumishi wa TAKUKURU Chalinze pamoja na Mikoa na Wilaya ambazo kuna majengo mapya kutunza na kuthamini majengo hayo pamoja na vitendea kazi vyote vilivyomo ili viweze kutumika hata na vizazi vijavyo.

Aidha, ametoa wito kwa taasisi ya TAKUKURU, Sekta za Umma na  Watanzania wote kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha fedha za Serikali zinazotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri zinatumika kulingana na malengo yaliyowekwa.

Amesema, utaratibu huo ni muhimu katika kuongeza uwazi na uwajibikaji na hivyo kuziba mianya ya rushwa na kuongeza ushiriki wa Wananchi katika kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa ipasavyo.

Akihitimisha hotuba yake, Waziri Kikwete amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila pamoja na watendaji wa taasisi hiyo kwa uadilifu na weledi unaoonekana katika usimamizi wa ujenzi wa jengo hilo.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye ujenzi wa majengo katika wilaya na mikoa mbalimbali nchini na hii ni kuonesha utashi wa Mhe. Rais katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali, Watumishi na Wananchi wakati akizindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali na Watumishi alipowasili kwa ajili ya kuzindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani

Baadhi ya Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali, Watumishi na Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuzindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispian Chalamila (kushoto) kabla ya Waziri huyo kuzindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge kabla ya Waziri huyo kuzindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani


Mkurugenzi Mtendaji wa TAKUKURU, Bw. Crispian Chalamila akitoa neno la utangulizi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kuzungumza na kuzindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Watumishi  wa TAKUKURU mara baada ya kuzindua jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.

Muonekano wa nje wa jengo la Ofisi za TAKUKURU lililopo Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani ambalo uzinduzi wake umefanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete leo tarehe 24 January, 2026.

Kaimu Mkurugenzi wa Milki, Bw. Frank Mkiranya akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuhusu utelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Jengo la Ofisi ya TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.

Baadhi ya Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali, Watumishi na Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuzindua Jengo la TAKUKURU ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akikata utepe alipokuwa akizindua Jengo la TAKUKURU Mkoa wa Pwani ambalo ni Kituo maalumu kilichopo katika Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.