Na. James K. Mwanamyoto-Babati
Tarehe 12 Julai, 2022
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi amesema watumishi wa umma nchini wana deni kubwa la kutoa
huduma bora kwa wananchi, kwasababu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameboresha
masilahi yao ili kujenga ari na morali ya kulitumikia taifa.
Mhe. Ndejembi amesema hayo,
wakati akizungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Mji Babati, akiwa
katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamozo zinazowakabili watumishi wa umma katika Halmashauri hiyo.
“Watumishi wa Halmashauri ya
Mji Babati mmeona namna Mhe. Rais alivyowapandisha madaraja na alivyolipa
malimbikizo yenu ya mishahara, hivyo mna deni kubwa kwa Mhe. Rais la kufanya
kazi kwa uadilifu pamoja na kutoa huduma bora kwa Watanzania,” Mhe. Ndejembi
amesisitiza.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa,
Serikali kazi yake kubwa ni kutoa huduma kwa wananchi, hivyo watumishi wa umma
wa Halmashauri ya Mji Babati pamoja na wa maeneo mengine wameajiriwa ili
kutekeleza azma hiyo ya Serikali na si kufanya biashara.
Akizungumzia changamoto ya
utendaji kazi wa baadhi ya watumishi wa umma nchini, Mhe. Ndejembi amesema
baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea bila ya kuwa na mpango kazi hivyo
kushindwa kutoa huduma bora kwa wananchi kama ambavyo Serikali imekusudia.
“Wengi wetu hapa hatuna mpango
kazi, tunafanya kazi kwa matukio wakati shida za wananchi ni nyingi sana na
tunao wajibu wa kuzitatua kwa wakati kwa kuwa na mpango kazi unaotekelezeka,”
Mhe. Ndejembi ameongeza.
Kwa upande wake, Mbunge wa Babati Mjini, Mhe. Pauline Gekul ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kufanya ziara ya kikazi jimboni kwake kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi walio katika jimbo lake ambao ndio watekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mhe. Gukul amesema, kazi
inayofanywa na Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius
Ndejembi ya kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma nchini,
inaongeza ari ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma ambao wana jukumu la
kumsaidia Mhe. Rais kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya
ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Mji Babati ya kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji
Babati (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi katika halmashauri hiyo
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi
hao.
Kaimu Mkuu wa Mkoa
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Lazaro Twange akitoa neno la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza
na watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati wakati wa ziara yake ya kikazi katika
halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi.
Afisa Utumishi wa
Halmashauri ya Mji Babati, Bw. Nemes Fungameza akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa Halmashauri ya Mji huo kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo
pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Mji Babati, Bw. Faraja Maduhu (aliyesimama)
akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi
(katikati) akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Mji Babati wakati wa ziara yake ya
kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi.
Mtendaji Kata wa Kata
ya Sigino Halmashauri ya Mji Babati,
Bi. Evaline Panga (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo
pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi.
No comments:
Post a Comment