Na. Veronica Mwafisi-Monduli
Tarehe 13 Julai, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ameadhimisha
kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake kwa kufanya kazi na kuhimiza wananchi na
watumishi wa umma nchini kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan ya KAZI IENDELEE.
Mhe.
Ndejembi amehimiza utekelezaji wa kaulimbiu hiyo kwa vitendo, akiwa katika
ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
katika Kijiji cha Naalarami wilayani Monduli.
“Nimeadhimisha
kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa kwa kufanya kazi siku nzima nikiwa katika
ziara ya kikazi mkoani Arusha, na nawashukuru wananchi wa kijiji cha Naalarami
kwa kunipatia zawadi ambayo itakuwa ni kumbukumbu kubwa maishani mwangu,” Mhe.
Ndejembi amesema.
Ameongeza
kuwa, katika kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa ametumia fursa hiyo kuwaasa
wananchi na watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii ili kuiishi kwa vitendo
kaulimbiu ya Mhe. Rais ya KAZI IENDELEE.
“Kwa
watumishi wa umma mliopo hapa, hakikisheni mnachapa kazi kwelikweli usiku na
mchana kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi hawa wa Kijiji cha Naalarami,”
Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amekagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba ya daktari inayojengwa kwa ufadhili wa OPEC (IV) kupitia uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akivalishwa
vazi la Kimasai na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Naalarami Halmashauri ya
Wilaya ya Monduli walipokuwa wakimpongeza kwa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya
kuzaliwa kwake, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwashukuru
walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Naalarami Halmashauri ya Wilaya ya Monduli mara
baada ya walengwa hao kumpongeza kwa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa
kwake, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kwenye Kijiji hicho.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akikata
keki kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.
No comments:
Post a Comment