Na. Veronica Mwafisi – Dar es Salaam
Tarehe
19 Julai, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amemtaka
Mkandarasi SUMA JKT kuhakikisha anakabidhi jengo la ofisi za karakana ya ndege
(HANGAR) kwa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA) tarehe 31 Julai, 2022, ili
kuiwezesha TGFA kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri wa anga kwa
viongozi wakuu wa nchi wakiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa.
Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo
hayo jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa ofisi za karakana ya ndege na kuridhika na hatua iliyofikiwa.
Mhe. Ndejembi amesema ofisi
yake inategemea tarehe 31 Julai, 2022 jengo la Ofisi ya Karakana ya Ndege litakabidhiwa
kwa TFGA, kwani TGFA inategemewa sana na Serikali katika kutoa huduma bora za
usafiri wa anga kwa viongozi wakuu wa kitaifa.
“Baada ya kufanya ukaguzi,
nimeridhika na kiwango cha ubora na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na mkandarasi
katika ujenzi wa jengo hili la ofisi za karakana ya ndege,” Mhe. Ndejembi
amefafanua.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa,
kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama anawapongeza Mkandarasi SUMA JKT, Mshauri
Mwelekezi DIT na Mzabuni TGFA kwa ujenzi uliozingatia ubora.
“Tumeona namna jengo lilivyo
la kisasa, kwani limewekewa vifaa vya kupambana na moto ikiwa ni pamoja na
kuwezesha matumizi mazuri ya umeme,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu
wa Wakala ya Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule amemshukuru Waziri
Jenista Mhagama na Naibu wake Mhe. Deogratius Ndejembi pamoja na wajumbe wa
bodi, kwa kufanya ziara za kukagua maendeleo ya ujenzi katika nyakati tofauti,
lengo likiwa ni kuhimiza ukamilishaji wa ujenzi wa ofisi za karakana ya ndege
ambao hivi sasa upo katika hatua nzuri kutokana na ufuatiliaji wao.
Kukamilika kwa jengo la ofisi
za karakana ya ndege (HANGAR) kutaiwezesha TGFA kutekeleza majukumu yake
kikamilifu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Ndege za Serikali, Mhandisi John Nzulule (wa pili kutoka kushoto) kuhusu
ukamilishaji wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Karakana ya Wakala ya Ndege za
Serikali alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo
hilo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa
maelekezo kwa wakandarasi wa SUMA JKT na wabunifu majengo wa DIT kuhusu ukamilishwaji
wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Karakana ya Wakala ya Ndege za Serikali
alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo jijini
Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali, Mhandisi John Nzulule akielezea maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Karakana ya Wakala ya Ndege za Serikali wakati Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es Salaam.
Mbunifu
Majengo - DIT, Bw. Anderson Allan akifafanua jambo kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (wa kwanza kulia)
wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa kwanza kushoto) akitoka kukagua jengo la ofisi ya Karakana ya Wakala ya Ndege
za Serikali wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
jengo hilo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ndege za Serikali, Mhandisi John Nzulule
Mhandisi wa Umeme – DIT, Bw. Adam Liwondo (wa kwanza kushoto)
akimuonesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kutoka kushoto) maeneo ambayo
umeme utapita wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es
Salaam.
Muonekano wa jengo la ofisi ya Karakana ya Wakala ya
Ndege za Serikali linaloendelea kujengwa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment