Tuesday, July 5, 2022

WALENGWA WA TASAF WAMSHUKURU RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUBORESHA MAISHA YAO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Nangombo, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, Bi. Mariana Mkwaila alipokuwa akieleza namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake ikiwemo kujenga nyumba ya kisasa wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Jenista iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Serikali wakiangalia nyumba ya mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Bi. Mariana Mkwaila wa Kijiji cha Nangombo Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma aliyoijenga kupitia ruzuku ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha Nangombo, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha Nangombo, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfumo wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. John Steven akitoa salamu za TASAF kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, Mzee Hilo Mbawala alipokuwa akieleza namna TASAF ilivyowezesha kuboresha maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Jenista iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, Bibi Elvina Haule alipokuwa akieleza namna TASAF ilivyowezesha kuboresha maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Jenista iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.


 

No comments:

Post a Comment