Sunday, July 3, 2022

MHE. JENISTA AELEKEZA VIKUNDI 450 VYA VALENGWA WA TASAF VYA AKIBA NA MIKOPO KUKOPESHWA FEDHA ZA HALMASHAURI ZISIZO NA RIBA MKOANI IRINGA

Na. James K. Mwanamyoto-Iringa

Tarehe 03 Julai, 2022 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amemtaka mratibu wa TASAF mkoani Iringa kuhakikisha vikundi 450 vya walengwa wa TASAF vya akiba na mikopo vinaingizwa kwenye mpango wa kukopeshwa fedha za Halmashauri zisizo na riba ili kuviwezesha vikundi hivyo kuboresha maisha yao. 

Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo, wakati akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kata ya Kitwiru wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mpango huo katika manispaa hiyo.

“Mratibu wa TASAF mkoa, Mhe. Diwani na watendaji wa TASAF makao makuu mliopo hapa hakikisheni vikundi hivi 450 vya walengwa wa TASAF vya akiba na mikopo kupewa kipaumbele cha kuingizwa kwenye mpango wa kukopeshwa fedha za Halmashauri zisizo na riba,” Mhe. Jenista amesisitiza. 

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, kipaumbele cha kuotoa mikopo kwa walengwa wa TASAF katika halmashauri zote nchini, ndio maagizo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa lengo la kuwawezesha walengwa wa TASAF kuanzisha miradi ya kilimo, ufugaji na shughuli nyingine za ujasiriamali ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa walengwa hao. 

Aidha, Mhe. Jenista alitoa fursa kwa walengwa wa TASAF wa Kata ya Kitwiru kueleza namna mpango wa TASAF ulivyowanufaisha, mmoja wa walengwa hao Bi. Joyce Mgonzo amesema kuwa ruzuku aliyoanza kupokea mwaka 2015 imemuwezesha kupata mtaji wa kufuga kuku wa kisasa 200 wa mayai na hatimaye kupata tuzo ya ufugaji bora mwaka 2021 aliyoipata jijini Mbeya kwenye Maonesho ya Siku ya Wakulima (Nane Nane). 

Naye, mlengwa mwingine wa TASAF katika kata ya Kitwiru, Mzee Ndalingwa Mwindichuma amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza mpango wa TASAF ambao umemuwezesha kufuga mbuzi 4, ng’ombe 1, kuku 8 na sungura 7, hivyo amemtakia Mhe. Rais maisha marefu kwa kumuwezesha kupitia TASAF.

 

Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manipaa ya Iringa, Bi. Joyce Mgonzo akieleza namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Bw. John Steven akitoa salamu za TASAF kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Bi. Stella Kyando akiwasilisha taarifa ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Mzee Ndalingwa Mwindichuma akieleza namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akicheza ngoma ya asili na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kata ya Kitwiru, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mara baada ya kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.


 

No comments:

Post a Comment