Na. Veronica Mwafisi - Babati
Tarehe 12 Julai, 2022
Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka
Walengwa wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini kuboresha maisha yao kupitia
ruzuku wanayopewa ili kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya
kuzikwamua kaya maskini kutoka katika lindi la umaskini.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo
kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini alipokuwa akizungumza na walengwa
hao wa Mtaa wa Arri waloiopo Kata ya Nangara Babati akiwa katika ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango huo katika Halmashauri ya Mji wa Babati.
Mhe. Ndejembi amewataka
walengwa kujiuliza namna Mhe. Rais anavyojitoa katika kutoa fedha ili kuzikwamua
kaya maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwani angeliweza
kuzielekeza fedha hizo katika shughuli nyingine za maendeleo.
“Mnaopokea ruzuku ya TASAF, ni
jukumu lenu kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuhakikisha mnazitumia vema fedha za ruzuku katika kuboresha maisha yenu kama
alivyokusudia,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe. Ndejembi amekemea kitendo
cha walengwa wa TASAF kutumia ruzuku wanayopewa katika anasa kama vile kunywa
pombe, jambo ambalo ni kinyume na lengo la Serikali la kuanzisha Mpango huo wa
Kuzinusuru Kaya Maskini nchini.
Kwa upande wake mmoja wa
walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Arri kata ya Nangara Halmashauri ya Mji Babati,
Bi. Lyidia Kaaya amesema ruzuku ya TASAF imemuwezesha kuboresha maisha yake
kwani alianza kufuga kuku na baadae kukodi shamba kwa ajili ya kilimo na
alipovuna aliuza mazao na kupata fedha zilizomuwezesha kujenga nyumba anayoishi
hivi sasa.
Naye, Mlengwa mwingine Bi.
Hellena Philemon ameishukuru TASAF kwa kumboreshea maisha yake, ambapo amewezeshwa
kusomesha watoto na kuboresha nyumba yake kwani kabla ya kuanza kupokea ruzuku
hakuweza kumudu gharama za masomo na kukarabati nyumba yake.
Aidha, Mwakilishi wa
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Oscar Maduhu amesema kuwa, TASAF imeona
mafanikio makubwa ya walengwa wengi
waliotumia ruzuku vizuri kuboresha maisha yao kupitia shughuli
mbalimbali za kiuchumi, na wapo wachache wanaosuasua hivyo TASAF inaendelea
kutoa elimu ya namna bora ya kutumia ruzuku ili kuboresha maisha yao.
Bw. Maduhu amesema, Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan bado anaendelea kutoa fedha za kutosha kuwezesha Mpango wa
Kuzinusuru Kaya Maskini nchini, hivyo TASAF itaendelea na uratibu wa
kuhawilisha kwa utaratibu wa mpango ili ziwafikie walengwa waliokusudiwa.
Walengwa wa Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini nchini katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakimshukuru, Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kuboresha maisha yao kupitia ruzuku
inayotolewa na TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza
na walengwa wa TASAF na wananchi wa Kijiji cha Arri, Kata ya Nangara, Halmashauri
ya Mji Babati wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini kwenye Halmashauri hiyo.
Walengwa
wa TASAF wa Kijiji cha Arri, Kata ya Nangara, Halmashauri ya Mji Babati
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri
huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwenye
Halmashauri hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati, Bi. Rena Urio akitoa taarifa ya
utekelezaji wa Mpango wa TASAF ya Halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri
huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika
Halmashauri ya Mji Babati.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Arri, Kata ya Nangara, Bi. Justine
Msuya akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ya
kijiji chake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa
Mpango wa TASAF katika Halmashauri ya Mji Babati.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Oscar Maduhu akitoa salamu za TASAF kwa
walengwa wa TASAF Kijiji cha Arri, Kata ya Nangara wakati wa ziara ya kikazi ya
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo
pichani) yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa TASAF katika Halmashauri
ya Mji Babati.
Mlengwa
wa TASAF wa Kijiji cha Arri, Kata ya Nangara, Halmashauri ya Mji Babati, Bi. Lyidia
Kaaya akieleza namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake, wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi yenye
lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika
Halmashauri ya Mji Babati.
Mlengwa
wa TASAF wa Kijiji cha Arri, Kata ya Nangara, Halmashauri ya Mji Babati, Bi.
Hellena Philemon akieleza namna TASAF ilivyomuwezesha kuboresha maisha yake
wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi yenye
lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri
ya Mji Babati.
No comments:
Post a Comment