Tuesday, July 5, 2022

WATENDAJI SERIKALINI WAJENGEENI UWEZO WATUMISHI WENU ILI KUTATUA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA WATAALAMU-Mhe. Jenista

Na. James K. Mwanamyoto-Nyasa na Mbinga

Tarehe 05 Julai, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewataka Watendaji Serikalini kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wanaowasimamia kwa lengo la kutatua changamoto ya upungufu wa wataalamu katika maeneo yao ya kazi. 

Mhe. Jenista amesema hayo kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua kero na changamoto zinazowakabili watumishi wa umma mkoani humo. 

Mhe. Jenista amehoji kwanini Watendaji Serikalini wamekuwa wakilalamika upungufu wa wataalamu wakati wanao watumishi wanaotekeleza majukumu kwenye maeneo yenye upungufu wa wataalamu ambao wanahitaji kupatiwa mafunzo ili kuwa na sifa stahiki za kutumikia nafasi hizo. 

“Fanyeni maamuzi kwa kuchagua watumishi wenye uwezo wa kuzitumikia nafasi hizo za kitaalamu, waombeeni kibali cha kuwaweka kwenye mpango wa mafunzo, wakihitimu mafunzo hayo warejee kutatua changamoto ya upungufu wa wataalamu katika maeneo yenu ya kazi.” Mhe. Jenista amesisitiza. 

Aidha, amewataka Watendaji hao kuhakikisha watumishi wote watakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kutatua changamoto ya uhaba wa watalaamu pindi watakapohitimu kurejea katika vituo vyao vya kazi badala ya kuomba uhamisho. 

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, Watendaji ndio walezi wa watumishi, hivyo wanapaswa kujisikia fahari kuwapeleka kwenye mafunzo watumishi ili waongeze ufanisi kiutendaji na kuwa na sifa stahiki zitakazowezesha kutatua changamoto ya upungufu wa wataalamu. 

Mhe. Jenista yuko mkoani Ruvuma kwenye ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kutatua changamoto zinazowakabili ili kuboresha utendaji kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.


Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Kanali Laban Thomas, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Wilaya yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Stephen Ndaki wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza hoja za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.



Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Bw. George Mpanda, akiwasilisha hoja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Halmashauri ya Mji Mbinga na taasisi nyingine za Serikali mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kanali Laban Thomas na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw. Stephen Ndaki.


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Halmashauri ya Mji Mbinga na taasisi nyingine za Serikali mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo mkoani Ruvuma iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi hao.


 

No comments:

Post a Comment