Na. James K. Mwanamyoto-Monduli
Tarehe 14 Julai, 2022
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi amewaasa watumishi wa umma kuwa na maadili ili kujenga taswira
nzuri ya Serikali kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zitolewazo
na taasisi za umma nchini.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo
kwa watumishi wa umma nchini, wakati akizungumza na watumishi wa umma wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, akiwa katika ziara ya kikazi yenye lengo la
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamozo zinazowakabili watumishi wa umma
katika Wilaya hiyo ya Monduli.
Mhe. Ndejembi amesema
watumishi wa umma ndio kioo cha jamii, na ni taswira ya Serikali katika jamii,
hivyo wanapaswa kuwa na maadili mema yatakayolinda haiba ya Serikali na utumishi
wa umma kwa ujumla.
“Mtumishi wa umma hapaswi kuwa
mlevi wa kupindukia au kuwa na tabia ambazo hazipendezi katika jamii
inayokuzunguka, kwani tabia hizo zinaharibu taswira nzuri ya utumishi wa umma,”
Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Aidha, Mhe. Ndejembi amewataka
watumishi wa umma kuzingatia utunzaji wa siri za Serikali wakati wa utekelezaji
wa majukumu yao ya kila siku, ili taarifa na nyaraka za Serikali ziendelee kuwa
katika mikono salama ya Serikali yenyewe.
“Watumishi wa umma hakikisheni
mnatunza siri zote za Serikali mnazozifahamu kupitia utendaji kazi wa shughuli
zenu za kila siku, ili kuviishi viapo vyenu mlipoajiriwa,” Mhe. Ndejembi
amehimiza.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Monduli, Mhe. Frank Mwaisumbe amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kuhimiza
uadilifu kwa watumishi wa wilaya yake, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na
ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Naye, Afisa Maendeleo ya
Jamii, Bi. Rose Mhina kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kusikiliza kero na changamoto
zinawakabili na kuzifanyia kazi papo kwa hapo, ikiwa ni pamoja na kutoa
ufafanuzi wa hoja mbalimbali za kiutumishi walizoziwasilisha.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya
ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa lengo
la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Monduli (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi katika
halmashauri hiyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi hao wa umma.
Watumishi
wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi hao wa umma.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Frank Mwaisumbe akitoa neno la
utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza
na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya yake, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi. Restiel
Mselli (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo
pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga
kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa
halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi
(Wakwanza kushoto) akisikiliza hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na
kutatua changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli.
Mtumishi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Monduli, Bw. Emmanuel Kipimo (aliyesimama) akiwasilisha hoja kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya
Naibu Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto zinazowakabili
watumishi wa halmashauri hiyo ya Monduli.
Afisa Maendeleo ya
Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Bi. Rose Mhina akitoa neno la
shukurani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya Naibu
Waziri huyo iliyolenga kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi wa umma wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Monduli.
No comments:
Post a Comment