Na. Veronica Mwafisi-Sumbawanga
Tarehe 18 Januari, 2022
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi amewahimiza Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga kuwajali wateja (custumer care)
pindi wanapofuata huduma ili kujenga taswira nzuri ya Serikali kwa umma.
Mhe.
Ndejembi ametoa wito huo kwa Watumishi wa Umma wilayani Sumbawanga, wakati wa
kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mhe.
Ndejembi amesema, kumekuwa na mtizamo hasi kuwa katika Utumishi wa Umma baadhi
ya watumishi hawawajali wateja jambo ambalo halijengi taswira nzuri ya Serikali
kwa wananchi.
Hatuna
budi kuwajali watumishi wenzetu tunaowahudumia na wananchi ambao ndio walengwa
wakuu wa huduma zinazotolewa na taasisi za umma, Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe.
Ndejembi ameongeza kuwa, Serikali haifanyi biashara, hivyo lengo lake kuu ni
kutoa huduma bora kwa wananchi ili wanufaike na uwepo wa Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imedhamiria
kuwapatia huduma stahiki.
Akizungumzia
kuhusu mienendo ya Watumishi wa Umma, Mhe. Ndejembi amesema ni lazima izingatie
miiko na maadili ya Utumishi wa Umma ili kulinda na kujenga taswira nzuri ya
Serikali kwa umma.
“Tusiwe
wa kwanza kuvunja Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma iliyopo,
hivyo ni lazima tufanye kazi kwa uadilifu,
Mhe. Ndejembi amehimiza.
Aidha,
Mhe. Ndejembi amesema kwamba hakuna wakati mzuri kama huu wa utawala wa Serikali
ya Awamu ya Sita kwa Watumishi wa Umma, hivyo watumishi wanapaswa kuunga mkono
juhudi za Mhe. Rais za kuhimiza masilahi yao kwa kutekeleza majukumu ya kila
siku kikamilifu.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga,
Mhe. Sebastian Waryuba amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi wa wilaya yake na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo aliyoyatoa.
Amesema
ili wananchi wa Manispaaa ya Sumbawanga wapate faraja ni lazima kuzingatia maelekezo
yaliyotolewa na Mhe. Ndejembi ili kufikia azma ya Mhe. Rais ya kuboresha huduma
zinazotolewa na Serikali kwa wananchi.
Mhe. Ndejembi
amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya Sumbawanga yenye lengo la
kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma wa Halmashauri hiyo, ikiwa ni pamoja
na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
(hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao wilayani humo chenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi
ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakimsikiliza Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga, Mhe. Sebastian Waryuba akimshukuru Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi kwa kufanya ziara ya kikazi wilayani Sumbawanga yenye lengo la
kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma wilayani humo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya
halmashauri yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa kikao kazi cha Naibu
Waziri huyo na Watumishi wa Wilaya hiyo, chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji
kwa Watumishi wa Umma wilayani Sumbawanga.
Mtumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Bi. Ipyana Masebo akiwasilisha
changamoto ya kiutumishi inayomkabili kwa Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya
Naibu Waziri huyo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akisikiliza hoja ya mmoja wa watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sumbawanga (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi
wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Afisa
Utumishi wa Halmashauri ya Sumbawanga, Bw. Samson Medda (Aliyesimama) akijibu
hoja iliyoulizwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati wa kikao kazi chake na
watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment